HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 03, 2024

Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Dodoma yaandaa mpango wa dharura utoaji huduma kwa wanachama wa NHIF

 Na Jasmine Shamwepu, Dodoma



Mganga Mfawidhi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma na Mwenyekiti wa Waganga wafawidhi Hospitali za Rufaa za mikoa Tanzania bara Dkt. Ernest Ibenzi ameeleza kuwa katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Dodoma kutakuwa na Mpango wa dharura wa utoaji huduma kwa wanachama wa NHIF kufuatia baadhi ya Hospitali nchini kusitisha huduma kwa wanachama wa NHIF.



Dkt. Ibenzi amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari ameeleza kuwa Hospitali imefanikiwa kuhamia kwenye kitita kipya cha mafao cha mwaka 2023 kilichopendekezwa na NHIF ambapo huduma zinaendelea kutolewa.


Aidha amesema Uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Dodoma umekuja na Mpango wa dharura wa kutoa huduma kwa wanachama hao ili waweze kuwa na mwendelezo wa huduma hizo.

Pia ameongeza kuwa Hospitali hiyo imeongeza muda wa kuona wagonjwa na kuwahudumia kwa wakati katika kliniki zote kwa saa 24.

Katika hatua nyingine ameeleza kuwa Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Dodoma kama mmoja wa watoa huduma hapa nchini wamejipanga vyema kutoa huduma bora kwa wananchi na itaendelea kufuatia utendaji wa kitita hicho ili kubaini changamoto zitakazojitokeza na kuziwasilisha katika Mamlaka husika.


No comments:

Post a Comment

Pages