HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 28, 2024

MHE EDWARD MPOGOLO AIPONGEZA ACB BENKI KUWA SEHEMU YA UKUAJI UCHUMI KWA TAIFA

NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM



MKUU wa Wilaya ya Ilala Mhe Edward Mpogolo, ameipongeza ACB kwa kuwa sehemu ya ukuwaji wa uchumi wa Tanzania kwa kutoa huduma nzuri za kifedaha ikiwemo mikopo yenye riba nafuu na kutoa ajira.


Pongezi hizo amezitoa Jijini Dar es salaam na kuahidi kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaendelea kuwa karibu na taasisi za fedha hususan benki ya Akiba katika kuinua uchumi wa nchi na kuleta maendeleo katika jamii.

Aidha Mhe. Edward Mpogolo ameipongeza  ACB kwa kuandaa hafla ya kufuturisha wateja, Wafanyakazi na wadau mbalimbali wa Benki hiyo iliyofanyika Jijini Dar es Salaam katika hoteli ya Serena tarehe 25 Machi, 2024

 “Licha huduma ya kifedha mnayoitoa bila kujali kuwa mtapata hasara mmefany jambo lenye upekee wake kwani kitendo cha kufuturisha  ni ibada  ambayo mwanadamu  aliyetunukiwa zaidi anatoa kwa wengine na atapata thawabu kwa kufanya hivyo pia baraka kutoka kwa mwenyezi Mungu ”


 

No comments:

Post a Comment

Pages