HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 02, 2024

WARIOBA KIKWETE NA KINANA WAMMWAGIA SIFA ALHAJI ALI MWINYI

Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete  akizungumza kwenye hafla hiyo

Bi Khadija Mwinyi  (Mjanewa marehemu) akitoa heshima zake mbele ya jeneza  la Hayati Mwinyi.


 Mwili wa aliyekuwa Rais wa Tanzania wa Awamu ya Pili Hayati Ali Hassan Mwinyi ukipita katika eneo la Magomeni wakati ukielekea katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam ambapo uliagwa kitaifa. (Picha na Rashid Shoti).




Na Khadija Kalili 

 

RAIS Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa  awamu ya nne  Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete    amesema kuwa Hayati Alhaji Ali Hassan  Mwinyi alikua Kiongozi asiyejikwaza,alikua mtu  mwenye mapenzi na watu wote.


Kikwete amesema hayo leo Machi mosi alipozungumza na viongozi  mbalimbali pamoja na waombolezaji  waliohudhuria hafla ya  kumuaga  kitaifa Hayati Mwinyi kwenye Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.

"Mwinyi  aliishi maisha  ya kawaida  ya uungwana ,alikua msikivu na alikua ni mtu wa kupokea  maoni na zaidi ya yote  alinifundisha  kuwa  na maamuzi hasa  kwenye vitu vyenye  maslahi ya taifa yeye ndiye baba wa mageuzi ya uchumi na kisiasa hapa nchini"amesema Rais Mstaafu Kikwete.

Naye Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza  wa Rais wa awamu ya pili Mstaafu Joseph  Warioba  akimzungumzia Hayati Mwinyi amesema kuwa  "Leo  ni siku ya  majonzi ya kyondokewa  na mzee Mwinyi  lakini  pia ni siku ya  furaha  ya kusherehekea  maisha  yake  kwa mengi aliyoyafanya wakati alipolitumikia taifa  hili,kwani amekuwa na juhudi nyingi  za kuleta  maendeleo hasa kwenye nyanja ya kiuchumi na kisiasa"amesema  Warioba. 


Wakati huohuo  Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Abdulrahman Kinana amemuelezea Hayati Mwinyi  kwa kusema kuwa "Sote ni  mashahidi kwamba  Hayati Ali Mwinyi  alifanya jitihada za kuitoa nchi ya Tanzania  kwenye mfumo wa chama kimoja  kwenda  kwenye mfumo wa vyama vingi" amesema Kinana.

Ameongeza kwa kusema kuwa suala hili halikuwa rahisi  vilevile alitupeleka  kwenye uchumi  huria  alifanya yote haya  mengine mengi  huku akimshirikisha Hayati baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere  kwa lengo la kuhakikisha  kwamba  mabadiliko yanafanyika kwa utulivu na kulinda  amani na utulivu wa nchi.


Kabla ya kupelekwa Uwanja wa Uhuru mwili wa  Alhaji Mwinyi umeswaliwa katika msikiti wa BAKWATA na  maziko yatafanyika kesho Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

Pages