HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 25, 2024

MNYAMA APIGA CHAFYA MUUNGANO CUP

Na John Marwa


BAADA ya ukame wa dakika 360 pasi na ushindi, mnyama Simba wa Msimbazi amefufuka kwa kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya KVZ, katika michuano maalumu ya Kombe la Muungano ikiwa sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 60 ya Muungano.

Ni kama kicheko kwa mgonjwa aliyekuwa ICU lakini bao la Dakika 25' zimetosha kwa Freddy Koublan kuwainua vitini mashabiki wa mnyama Simba katika Uwanja wa New Amaan complex, visiwani Unguja, Zanzibar. Na kuwafanya kupiga chafya ya uzima mpya.


Dakika 90'+4 Israel Mwenda anaihakikishia Simba kutinga hatua ya fainali ya michuano hiyo ikiwa ni marejeo ya baada ya kufanyika miaka 20 iliyopita.


Nusu fainali ya pili inachezwa leo, ambapo wageni wa mashindano hayo Azam FC watakapokabiliana na KMKM majira ya saa 2:15 usiku.


Kama mnyama Simba atafanikiwa kutwaa taji hilo itakuwa mwanzo mwema wa kuendea msimu ujao wakiwa na mtazamo chanya wa kutatua matatizo yao na kukijenga kikosi chao na kuwarejesha kwenye mbunga yao ya kula nyama na maziwa.
Mwisho

No comments:

Post a Comment

Pages