HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 25, 2024

TETESI ZA MAJUUU LEO APRIL 25


Manchester United wanavutiwa na mshambuliaji wa Brentford na England Ivan Toney na wanaamini kwamba mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 ataleta uzoefu na uongozi kwenye kikosi chao (90min).


Hata hivyo, Tottenham wanaweza kumnunua Toney iwapo kutakuwa na ushindani wa kutosha kuipata sahihi yake na kutoa pauni milioni 45. (GivemeSport).


Wakati huo huo Manchester United inalenga kuwaachilia wachezaji 12 msimu huu wa joto, akiwemo fowadi wa Uingereza Marcus Rashford, 26, na kiungo wa kati wa Brazil Casemiro, 32. (Mirror).


Huko London Mustakabali wa Mauricio Pochettino kama meneja wa Chelsea upo katika mizani na unaweza kutegemea iwapo anaweza kufuzu kwa shindano la Uropa kwa msimu ujao (Times)


Nae Mshambulizi wa Napoli Victor Osimhen, 25, anakaribia kujiunga na Paris Saint-Germain , lakini mshambuliaji huyo wa Nigeria pia ameivutia Chelsea . (Il Mattino - kwa Kiitaliano).


Matajiri wa Newcastle United wanaongoza katika kinyang'anyiro cha kumsajili beki wa kati wa Sporting Lisbon mwenye umri wa miaka 20 Ousmane Diomande, ambaye ana kipengele cha kutolewa cha euro 80m (£68.7m). (A Bola - kwa Kireno).


Nao Tottenham wako katika nafasi nzuri ya kumsajili kiungo wa kati wa Uingereza Conor Gallagher, 24, kutoka Chelsea msimu huu - licha ya kumezewa mate na Newcastle. (Football Insider).


Habari hizi ni kwa msaada wa mtandao na Tovuti ya bbc.swahili

No comments:

Post a Comment

Pages