HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 27, 2024

MNYAMA NA KITENDAWILI CHA MUUNGANO

 

Na John Marwa 

Wakati Taifa likisubiri kushuhudia Fainali ya Kombe la Muungano baada ya miaka 20 kupitia Mnyama Simba ambapo anamenyana na Azam FC wana kitendawili cha kujibu mashabiki zao kwa kutwaa taji hilo ama kulipoteza.

Ni Fainali ambayo hakuna wanachohitaji wana Lunyasi zaidi ya kusikia ama kushuhudia timu yao ikinyanyua kwapa usiku wa leo katika Visiwa vya Marashi ya karafuu ambapo Fainali hiyo itarindima  katika Viwanja vya New Amani Complex.

Wakizungumza kuelekea mchezo huo Kocha Msaidizi wa Simba Suleiman Matola na Nahodha Msaidizi Mohamed Hussein wamekiri mchezo kuwa mgumu na Azam ni mpinzani mgumu ila wanaingia kusaka ushindi tu na si kingine.

“Itakuwa mechi ngumu, Azam ni timu bora lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda. Hii ni fainali na siku zote haiwezi kuwa nyepesi kwahiyo tumejipanga kuwakabili.”- Kocha Msaidizi, Seleman Matola.

“Tunaiheshimu Azam lakini tupo tayari na tutaingia uwanjani kwa lengo la kutafuta ushindi ili tuibuke na ushindi.”- Nahodha Msaidizi, Mohamed Hussein.

Mwisho

No comments:

Post a Comment

Pages