HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 17, 2024

Mrajisi Vyama vya Ushirika 'akalia kuti kavu'

 Na Jasmine Shamwepu, DODOMA


WAZIRI wa Kilimo Hussein Bashe, amemwagiza Mrajisi wa Vyama vya Ushirika nchini Dk. Benson Ndiege kumaliza mara moja suala la wizi na ujambazi unaofanyika katika vyama hivyo vinginevyo nafasi yake itakua matatani.


Bashe, ameema hayo leo jijini hapa alipokuwa akifungua mkutano mkuu wa 14 wa wadau wa Kahawa nchini.

Ameseema, suala la wizi katika vyama vya ushirika nchini linapaswa kukomeshwa mara moja kwani limekuwa moja ya sababu ya kuwanyonya wakulima.


"Kuna vyama vya ushirika viongozi wake wamechukua fedha  shilingi milioni 200 za wanunuzi wa kahawa lakini wamegoma kurejesha fedha hizo wala kutoa kahawa na deni hilo lote linabebwa na wakulima.


"Nakuagiza Mrajisi wa vya vya ushirika wizi huu na ujambazi unaofanywa katika vyama hivi unakwisha mara moja na mimi Ma DG wengi wa wizara hii ambao nimewaondoa kwenye nafasi zao ni kwasababu nilikua nawaambia kama hivi lakini hawachukui hatua"alisema Bashe


Amesema, viongozi wote ambao wamehusika kwenye wizi ndani ya vyama vya ushirika wanapswa kufikishwa mahakamani kwa kosa la wizi na siyo madai kama ilivyo sasa.


"Inasikitisha sana kuona viongozi wamekula fedha na wanapofikishwa mahakamani wanafunguliwa shitaka la madai na mzigo wa deni lile wakulima wanalibeba halafu viongozi wanaendelea kudunda tuu mtaani ndiyo maana China watu kama hawa wanyongwa"alisema Bashe


Aidha, am sema vyama vingi vya ushirika licha ya viongozi wake kuwa wezi lakini vimekuwa ni sehemu ya kunyonya wakulima kwa kuweka tozo nyingi.


"Unakuta leo hii chama kimeweka tozo ya gunia,gharama za ulinzi, riba ya mkopo na wakulima wanakatwa bila kushirikishwa kuwa ni asilimia ngapi wanapaswa kukatwa"alisisitiza Bashe


Kadhalika, Bashe aliwata viongozi wa vyama vya ushirika kuandaa mahitaji ya wakulima na kuyawasilisha Bodi ya Kahawa ili yafanyiwe kazi.


"Kama kuna mahitaji ya mbolea,viuatilifu na mahitaji mengine andaeni mapema ili Bodi iyafanyie kazi ili kuondokana na tatizo la vyama vya ushirika kukopa fedha kwa wanunuzi wa kahawa na kuwabesha mzigo wa riba wakulima"alisema


Mwenyekiti wa Bodi ya Kahawa Prof. Aurelia Kamuzora, amesema malengo ni kuzalisha tani 300,000 za kahawa ifikapo mwaka 2025 kutoka tani 80 za hivi sasa.


Pia, Prof. Kamuzora aliwataka wakulima wa kahawa nchini kutumia mfumo rasmi wa uuzaji zao hilo na kujipesha na walanguzi ambao wamekuwa wakiwadanya kuuza kwa bei ya hasara.


Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge Viwanda,Bisahara,Kilimo na Mifugo Mariam Ditopile, ameema wataendelea kuisimamia serikali kutenga bajeti ya kutosha katika sekta ya Kilimo.


Ditopile, amesema ipo haja ya kuwekeza katika soko la ndani na kahawa ili kuwa na uhakika kwa wakulima tofauti na ilivyo sasa ambapo kiasi kinachouzwa nje kinaongezwa thamani na kurudi nchini kwa bei ya juu.



No comments:

Post a Comment

Pages