HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 17, 2024

Watoto zaidi ya milioni tano kupata chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi

 Na Jasmine Shamwepu, Dodoma



Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha elimu ya Afya kwa umma Dkt. Tumaini Haonga amesema Serikali kupitia Wizara ya Afya imepanga kuendelea utoaji wa chanjo kwa watoto zaidi ya milioni tano ya ugonjwa wa Saratani ya mlango wa kizazi (HPV) kwa mabinti wa miaka tisa hadi kumi na nne ili kuwakinga na vimelea vya ugojwa huo.


Ameyasema hayo wakati wa semina ya waandishi wa habari kuhusu chanjo ya Saratani ya mlango wa kizazi jijini Dodoma na kuongeza kuwa chanjo ya saratani ya HPV itatolewa dozi moja ambapo awali ilikuwa ikitolewa kwa watoto wenye umri wa miaka kumi na minne tu kwa dozi mbili na kuvitaka vyombo vya habari  kutumia  taaluma zao kuhamasisha na kuelimisha na kuwapa ufafanuzi wananchi juu ya masuala mazima ya afya hususani kuhusu ugonjwa wa saratani na mlango wa kizazi na chanjo yake kwa sababu wananchi wengi wanategemea kupata taarifa kupitia vyombo vya habari.



Kampeni hii itafanyika nchi nzima kuanzia tarehe 22 hadi 28 April 2024 wakati wa maadhimisho ya wiki ya chanjo Afrika katika vituo vya kutolea huduma za chanjo na shuleni

Kufuatia utoaji wa chanjo hiyo Kaimu Mkurugenzi wa kinga kutoka Wizara ya Afya Dkt.Tumaini Haonga amewaomba waandishi wa habari kuendelea kutoa elimu kwa Umma, kuendelea kufanya uchinguzi wa awali mara kwa mara juu ya saratani ya mlango wa kizazi.

"Zipo sababu mbalimbali ambazo kwa nyakati tofauti tumeendelea kusisitiza lakini kwa magonjwa haya ambayo yanazuilika kwa chanjo ni muhimu tuweke msisistizo mkubwa kwa wananchi kutumia nafasi ya kupata chanjo kama nafasi pekee ya kupata kinga ya uhakikaa"amesema



Aidha Dkt.Haonga amewaomba waandishi wa habari kuendelea kutoa ufafanuzi kwa jamii kuhusu sintofahamu au ya maswali ambayo wananchi hawana ufahamu juu ya saratani ya mlango wa kizazi

"Tuna wananchi ambao kwa bahati mbaya hawajapata fursa ya kufahamu masuala ya msingi kuhusu kanuni muhimu za afya,sasa kundi hili la wananchi wao wanategemea taarifa ,na taarifa wanazipata kutoka kwa wananchi wenzao,taarifa wanazipata kutoka Kwenye mitandao ya kijamii,taarifa watazipata kutoka Kwa wanahabari "amesema


Pia Dkt.Haonga amesisitiza kwa kuwaomba wanahabari kuisaidia Serikali kuendelea kutoa ufafanuzi kuhusu masuala haya ya chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi na chanjo nyingine.

Kwa Upande wake Bi.Lotalis Gadau Mratibu wa chanjo Wizara ya Afya amesema kuwa utoaji wa chanjo katika kampeni hii utahusisha vituo vya kutolea huduma za Afya,huduma za mkoba,shule na timu za uchajaji zitakuwa kwenye vituo kwa siku nne.

Kuhusu lengo la kampeni hii.Lotalis amesema kuwa ni kuwapa kinga mabinti wa miaka 9 hadi 14 na kuzuia kuenea kwa maambukizi ya saratani ya mlango wa kizazi kwa Wanawake hapo baadae.

Pia amesema wiki ya chanjo ina lengo la kuwatafuta walengwa wote waliokosa kupata chanjo.

Ameongeza kuwa chanjo zinatolewa katika vituo vya huduma za Afya bila malipo

"Ni muhimu kwa mzazi/mlezi kuhakikisha mtoto anakamilisha chanjo zote kulingana na ratiba,chanjo zote ni salama zimethibitishwa na Wizara ya Afya na Shirika la Afya Duniani"amesema


Uzinduzi wa chanjo hii ya mlango wa kizazi Kitaifa utafanyika Mkoani Mwanza tarehe 22 April,2024 na kauli mbiu ni "Jamii iliyopata chanjo,Jamii yenye Afya


No comments:

Post a Comment

Pages