HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 17, 2024

SERIKALI ZA TANZANIA BARA, SMZ KUTENGENEZWA SHERIA YA UKAGUZI WA NDANI

Rais wa Taasisi ya Wakaguzi wa Ndani Tanzania (IIA), CPA Zelia Njeza (Kushoto) akimkabidhi zawadi maalumu,mgeni wa heshima, Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar, Dkt. Saada Mkuya Salum kuelekea mkutano Mkuu wa Shirikisho la Wakaguzi wa ndani Afrika (AFIIA) Jijini Arusha Tanzania, huku ajenda ya utawala Bora na matumizi ya tehama zikipigiwa chapuo.

Picha ya pamoja ya Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar, Dkt. Saada Mkuya Salum akiwa na viongozi mbalimbali wanaoshiriki Mkuu wa Shirikisho la Wakaguzi wa ndani Afrika (AFIIA) Jijini Arusha Tanzania, ambapo katika mkutano huo ajenda ya utawala Bora na matumizi ya tehama zikipigiwa chapuo.


Rais wa Taasisi ya Wakaguzi wa Ndani Tanzania (IIA), CPA Zelia Njeza (Wa pili kulia) akimkabidhi zawadi maalumu,mgeni wa heshima, Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar, Dkt. Saada Mkuya Salum (Wa pili kushoto) kuelekea mkutano Mkuu wa Shirikisho la Wakaguzi wa ndani Afrika (AFIIA) Jijini Arusha Tanzania, huku ajenda ya utawala Bora na matumizi ya tehama zikipigiwa chapuo.

Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar, Dkt. Saada Mkuya Salum akizungumza na wanahabari kuelekea mkutano Mkuu wa Shirikisho la Wakaguzi wa ndani Afrika (AFIIA) Jijini Arusha Tanzania.

SERIKALI  ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) na  Tanzania Bara zipo mbioni kukamilisha taratibu za kutengenezwa kwa sheria, kwa ajili ya ukaguzi wa ndani ili kuhakikisha kaguzi hizo zinaimarika zaidi, sanjari na masuala ya utawala bora.

Akizungumza katika mkutano wa 10 wa Taasisi ya Wakaguzi wa Ndani Tanzania(IIA),Waziri wa Fedha kutoka  Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ)Saada Salum Mkuya, alisema awali hakukuwa na sheria ya kaguzi za ndani kama ilivyo, ili ya Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

Alisema uwepo wa sheria hiyo ya ukaguzi wa ndani utawezesha kaguzi kufanyika zaidi kwakuzingatia sheria kanuni  na taratibu za ukaguzi ili kuhakikisha zinaendana na kasi ya mabadiliko ya teknolojia. 

Alisema utawala bora ni msingi wa kila kitu hivyo lazima wakaguzi wa ndani wafanye kazi kwa umakini ili kuhakikisha kaguzi zinaimarika zaidi kwa kuzingatia misingi ya utawala bora.

"Serikali hizi mbili zipo mbioni kukamilisha taratibu za kutengeneza sheria za ukaguzi wa ndani ili kuhakikisha kaguzi hizi zinafanywa kwa umakini zaidi lakini pia mkutano huu utafunguliwa Aprili 17 na Makamu wa Rais,Dk, Philip Mpango "

Alisema mkutano huo mkubwa wa AFIII 'African Federation of Institutes of Internal Auditors' unatarajia  kufunguliwa na Makamu wa Rais Dk, Philip Mpango Aprili  17 mwaka huu na kushiriki washiriki mbalimbali kutoka nje ya nchi ambapo ni zaidi ya 500.

Alisema uwepo wa masuala ya usalama wa mitandao na akili bandia (IA) ni muhimu yakitumiwa katika kuimarisha mabadiliko ya kiteknolojia sanjari na kaguzi za ndani.

Naye Rais wa Taasisi ya IIA,Zelia Njeza alisema mkutano huo ni muhimu katika masuala ya ukaguzi hususan wakaguzi wa ndani Afrika na kuwakunzia wameanza na viongozi wa taasisi za umma, wakurugenzi,wajumbe wa bodi ili kuleta chachu ya utendaji kazi katika masuala ya kaguzi na maamuzi kwenye vikao.

"Sisi kwetu haya ni mafanikio makubwa kwani tutakuwa tumeileta Afrika na Dunia kiujumla kuja Tanzania kwa pamoja na kujionea nchi yetu inafanya kitu gani kwenye masuala ya ukaguzi  wa ndani," alisema.

Alisema tukio hilo la kukutanisha wananchi kutoka mataifa mbalimbali litakuwa ni fursa za kuunga mkono juhudi za serikali kupitia kwa Rais wa Tanzania, Samia Hassan Suluhu kuitangaza nchi nje ili kuvutia watalii kuitembelea Tanzania kwa shughuli za utalii.

Alisema lengo la mkutano huo wa siku tano ni kutathmini shughuli za kaguzi  pamoja na kuzungumza na wadau wa taasisi kutoa elimu kwa umma na pia kung'amua changamoto na namna ya kuzikabili.

"Tukiwa na sauti moja katika masuala ya ukaguzi hususan kaguzi za ndani kwa nchi za Afrika tutapiga hatua sanjari na kusaidia nchi zetu kuwa na sauti moja ikiwemo kutengeneza uwanda mpana wa mashirikiano kati ya Tanzania, Afrika na duniani kwajili ya kutatua changamoto mbalimbali ili kuleta mafanikio makubwa kwa nchi na kwa taasisi ambazo wakaguzi wa ndani wanafanyia kazi.

Naye mmoja kati ya washiriki wa mkutano huo,Profesa Esther Dungumaro alisema mkutano huo inatoa picha kwa wajumbe wabodi, wakurugenzi na wakuu wa taasisi kuamua mambo mbalimbali yanayohusu masuala ya fedha na mikakati dhabiti ikatakayosaidia taasisi kupata maendeleo zaidi.

No comments:

Post a Comment

Pages