HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 08, 2024

Bodi ya Ushauri ya Watoto Taifa yatakiwa kuwa na umoja- Waziri Pembe

Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mhe Riziki Pembe Juma ameitaka Bodi ya Ushauri ya Watoto Taifa kuwa na umoja moja katika mapambano ya vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia dhidi ya  Wanawake na Watoto.



 

Ameyasema hayo jana wakati alipokutana na bodi hiyo Ofisini kwake Kinazini Mjini Unguja. Amesema hivi sasa inaonekana watoto wa kiume kuharibiwa kwa kasi. Hivyo Mhe. Riziki amewataka wajumbe wa bodi hiyo kunganisha nguvu ya pamoja katika mapambano ya vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia dhidi ya  wanawake na Watoto.

 

Mhe. Riziki amefahamishwa kwamba Wizara anayoisimamia imeundwa kwa ajili ya kushughulikia masuala  mbalimbali ya kijamii nchini, ikiwemo masuala yanayowahusu watoto, hivyo ameitaka bodi hiyo kuhakikisha changamoto zinazowakabili watoto  kuziwasilisha katika Wizara hiyo ili kuweza kupatiwa ufumbuzi.

 

Aidha amewataka kuhakikisha wanabadilisha mitazamo ya baadhi ya watoto wanokataa kushiriki katika vikao au wito wowote kwa kuona kwamba hakuna malipo ya fedha  au zawadi kwani hali hiyo inaweza kutoa fursa kwa watu wabaya kutumia mwanya huo na kuwaharibu.

 

Amewahakikishia kuwa changamoto   zinazowakabili katika bodi kupitia Wilaya zao, Wizara itajitahidi kutazifanyia kazi kadiri hali itakavyoruhusu ili kuona mafanikio yanapatikana juu ya kunzishwa mabaraza hayo.


 

 

Naye Makamo Mwenyekiti wa bodi ya Ushaui Taifa ndugu Tatu Khamis Ramadhan ameelezea kufurahishwa kwake kwani ni  mara ya kwanza bodi hiyo kukutana na Waziri wao, na kuelezea changamoto zinazowakabili ikiwemo ndoa za utotoni,  baadhi ya vijiji kutofuatwa ipasavyo sheria ya mtoto sheria no.6 ya mwaka 2011 ambayo inaeleza haki za mtoto.

 

Hata hivyo ameiomba Wizara kuwapatia vyeti maalumu wajumbe au viongozi waliomaliza kutumikia mabaraza ya Watoto ili iwe ni uthibitisho kwao kwamba wamejitolea kutumikia taifa lao.

 

Pia wameomba kufanya uwezekano wa kuwekwa vituo vya one stop center katika hospitali mbalimbali ili iwe rahisi kupatiwa huduma za matibabu kwa waliopata tatizo la udhalilishaji.

No comments:

Post a Comment

Pages