HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 02, 2024

SIMBA SC WAKUBALI KUANZA UPYA!!


NA FARAJI MUSTAPHA


Hakuna mchawi zaidi yao wenyewe (wenye timu), kipindi hiki wanachokutana nacho ndio kinapaswa kuwa TURNING POINT.

Nimejaribu kupitia timu tatu za nafasi za juu kwenye NBC Premier League, Simba Sc ndio timu inayotia huruma katika maeneo yote matatu ya kiwanja ESPECIALLY eneo la ulinzi.

Ipo wazi kila timu LAZIMA iwe na wachezaji 11 wa kikosi cha kwanza,then wengine wtaaanzia mbao ndefu..

Nimepitia kwenye eneo la MABEKI WA KATI kwenye hizi timu tatu kuna kitu nimegundua.

YANGA SC na Azam Fc Wana BACKUP bora ya center backs kuliko Simba Sc.

Kwanini?

Nenda Yanga angalia mabeki wawili wa kati wanaoanza mara nyingi (Bacca+Job) halafu angalia bench kuna Gift Fred na Bakari Mwamnyeto hawakupi hofu kubwa endapo Bacca na Job wakikosekana.

Nenda Azam Fc,siku za karibuni wanacheza Fuentes Mendoza na Yannick Litombo Bangala,lakini pale mbao ndefu kuna Daniel Amoah,Manyama,waondoe Sebo na Malikou Nd'oye ambao wana pancha.. yoyote akipewa nafasi anaubonda vyema na hawa wanaonza mara kwa mara.

Njoo Simba Sc sasa, MABEKI WA KATI panga pangua ni Inonga na Che Malone halafu nje wapo Kazi na Kenedy Juma,ukitaka kuona mpishano wa viwango siku itokee Inonga na Che Malone wawe wote pancha halafu waanze Kenedy Juma na Kazi tena kwenye mechi yenye tension,hapo utaona vitu vingi vya utofauti na wale wanaoanza.

Simba Sc imeruhusu magoli 23 katika michezo 22 ya NBC Premier League msimu huu,kitu ambacho sio cha kawaida sana

Kujikwaa sio kuanguka, Simba Sc wanapaswa kufanya maboresho ya maana kila eneo ili waweze kurudisha makali kuja kuleta ushindani wa juu mbele ya Yanga inayoonekana kuwa kwenye kilele cha ubora.


No comments:

Post a Comment

Pages