HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 04, 2024

Mazingira Plus, TCCI wapanda miti kuelekea siku ya Mazingira Duniani


Afisa Misitu Wilaya ya Temeke Neema Daudi (katikati), akipanda mti katika Chuo cha Maafisa katika Kanisa la Jeshi la Wokovu jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Mazingira Plus, Abdallah Mikulu na kushoto ni Mkurugenzi wa Tanzania Cleanup and Conservation Initiative-TCCI, Salum Kingungo.

Baadhi ya wafanyakazi wa DHR wakishirikiana na HR Magret Mwambe (katikati), wakipanda mti kuelekea Siku ya Mazingira Duniani itakayofanyika Juni 5, 2024 hafla iliyoandaliwa na Taasisi ya Mazingira Plus kwa kushirikiana na Taasisi ya Tanzania Cleanup and Conservation Initiative-TCCI.

Kanali Colonel Mkami Asikofu Mkuu wa Kanisa la Jeshi la Wokovu Tanzania,akizungumza jijini Dar es Salaam leo katika makao Makuu ya Kanisa hilo, kuelekea siku ya Mazingira Duniani itakayofanyika kesho hafla iliyoandaliwa na Taasisi ya Mazingira Plus na Tanzania Cleanup and Conservation Initiative-TCCI.

Mkurugenzi wa Mazingira Plus, Abdallah Mikulu, akizungumza Makao Makuu ya Kanisa la Jeshi la Wokovu jijini Dar es Salaam katika kuelekea Siku ya Mazingira Duniani itakayofanyika kesho hafla iliyoandaliwa na Taasisi ya Mazingira Plus na Tanzania Cleanup and Conservation Initiative-TCCI.










No comments:

Post a Comment

Pages