Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam
Benki
ya Access Microfinance Tanzania Limited imesema kuanzia Juni 4 mwaka
huu imekuja na mabadiliko chanya ya chapa ya jina na kwamba kwa sasa
itatumbulika kwa jina la Selcom Microfinace Bank Tanzania Limited.
Aidha, baada ya kubadili jina kua Selcom Microfinance Bank Tanzania Limited imesema itahakikisha Wajasiriamali wa kati na wa chini wanawezeshwa kiuchumi ikiwemo kukuza biashara zao kupitia mikopo, benki hiyo imetenga Sh trilion1.6 ili kuwawezesha wajasiriamali hao.
Akizungumza
na wanahabari jijini Dar es Salaam Afisa Mtendaji Mkuu wa Selcom
Microfinance Bank Tanzania Limited Julius Ruwaichi amesema ubadilishaji
wa chapa ya jina unaonyesha dhamira ya kubadilika kulingana na mahitaji
ya wateja wao hivyo itajielekeza kutoa huduma zilizo sahihi na fasaha za
kifedha zilizojaa ubunifu mkubwa.
"Selcom
Paytech Limited, mwanahisa wetu mkubwa, anabeba jina linaloaminika
katika tasnia ya huduma za kifedha na malipo kwa zaidi ya miaka 22.
Selcom Paytech, ambayo ni maarufu kwa maendeleo na kutegemewa, imekuwa
mstari wa mbele katika ubunifu na uvumbuzi nchini. Tunapohamia Selcom
Microfinance Bank Tanzania Limited, tunaleta pamoja nasi kiwango kile
kile cha ari, kutegemewa, ubunifu na uvumbuzi ambacho umekuwa
ukiufurahia na kukidhi matarajio yako," amesema Ruwaichi.
Amebainisha kuwa kama
sehemu ya kuimarisha muonekao wao, Benki ya Selcom Microfinance
Tanzania Limited wataleta utambulisho mpya kwa muonekano wake na rangi
kuu za muonekano zitabadilika kuwa nyekundu, nyeupe na nyeusi na kwamba
sura ya nje ya mwonekano wao inabadilika, huku ahadi zao dhabiti za
huduma zilizoboreshwa zinazozidi matarajio yako na kukufanya wateja wawe
nao daima.
Amesisitiza kuwa wa
sheria zinazoongoza mabadiliko hayo hayataathiri haki au wajibu wowote
wa benki au kutoa kuathiri madai/mashauri yoyote ya kisheria na au
dhidi ya wadau wao, wala kanuni, kila kitu kitakuwa kinahama kutoka
Access Microfinance Bank Tanzania Limited hadi Selcom Microfinance Bank
Tanzania Limited.
Ameongeza kuwa katika kipindi cha Mwezi Mei, 2024 zaidi
ya vijana wakiwemo wakulima 200,000 na wafanyabishara wameweza kupatiwa
mikopo huku akibainisha tayari wameshafungua matawi katika mikoa ya
Iringa, Mbeya pamoja na Dar es Salaam.
Pia amesema mtaji
wa benki umefikia Sh Bilioni 8.6 na kwamba baada ya miwili ijayo
wamelenga kukuza mtaji hadi kufikia Sh bilioni 20 huku akifafanua Riba ya benki hiyo ni Asilimia 2 hadi 4.8 kutokana aina ya mkopo ya mteja anaouchukua.
No comments:
Post a Comment