HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 02, 2024

IDRISS ELBA AIBUKIA TAMASHA LA 27 LA ZIFF

Na Andrew Chale, Zanzibar

NYOTA wa filamu duniani kutoka Hollywood, Marekani, Idriss Elba jina lake limechomoza katika ufunguzi wa Tamasha la 27, la Filamu la Nchi za Jahazi (ZIFF) I Agosti, 2024 kufuatia Serikali ya Mapinduzi Zanzibar SMZ kutangaza kumpatia hekari 80, ilikujenga Studio ya kisasa ya Kimataifa.

Akifungua Tamasha hilo, Waziri wa Uwekezaji Zanzibar Shariff Ali Shariff amesema kuwa,  Serikali imejipanga kuhakikisha inakuza sekta ya filamu Visiwani Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.

"Tumempatia Idrisa Elba kule Kijiji cha Fumba hekari 80 ili kujenga kitu kama tunachokiona Bollywood, Nollywood.

....Zanzibar sijui sijui tutaiitaje "ZOLLYWOOD" au "ZALLYWOOD". Amesema Mhe Sharif Ali Sharif.

Aidha, Amesema kwamba jambo hilo lilimkaa kifuani muda mrefu hivyo bora amesema kila mtu afahamu namna Serikali ilivyojipanga katika kuendeleza sekta ya filamu Visiwani humo.

Itakumbukwa Nyota huyo raia wa Uingereza, Idrisa Elba anafanya uigizaji, utunzi na utayarishaji wa muziki, amefanya filamu mbalimbali ikiwemo "Luther", "Pacific Rim", "Mandela: Long Walk to Freedom", na "Thor" na zingine nyingi.

Itakumbukwa wakati ziara ya Rais Samia Suluhu Hassan akiwa  Davos, Uswisi, alikutana na Idris Elba, na kuongelea mipango ya kuwekeza studio kubwa ya Kimataifa ya filamu Tanzania.



No comments:

Post a Comment

Pages