HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 15, 2024

TALGWU YAISHUKURU SERIKALI KULIPA WATUMISHI MISHAHARA YAO KUPITIA MFUKO WA HAZINA

Na Magrethy Katengu, Dar es Salaam



CHAMA  cha Wafanyakazi wa serikali za mitaa Tanzania (TALGWU)  kimeishukuru serikali ilivyoridhia ombi lao la muda mrefu kwa kuanza utekelezaji wake mwezi Julai 2024 ambapo wanachama wao 445 kati ya 645 kulipwa mishara yao na kupitia mfuko  wa Hazina.


Shukrani hizo amezitoa Agosti 14 Jijini Dar es salaam na Katibu Mkuu wa Talgwu Raahidi Mtima ambapo amesema hiyo ni hatua kubwa serikali iliyochukuqa kwani inakwenda kuondoa kero za muda mrefu kuchelewa kwa mishahara na itaongeza ari na morali ya kufanya kazi hivyo ni budi na hao wanachama waliosalia 180 katika majiji na Manispaa ambao bado wanalipwa na mapato ya Halmashauri nao waanze kulipwa na hazina.


"Watumishi katika Halmashauri ambao mishahara yao ilikuwa inalipwa kupitia mapato ya Halmashauri Talgwu katika vikao na majadiliano mbalimbali na serikali mara kadhaa ilikuwa ikizungumzia changamoto kero na kadhia kubwa walizokuwa wanapitia ikiwemo kutolipwa mishahara kwa wakati,kutokopesheka,kukosa huduma ya matibabu mfuko wa NHIF kupata usumbufu wanapostaafu kutokana na makato yao kutowasilishwa kwa binadamu kwa wakati" amesema Katibu Mkuu.

Hata hivyo Talgwu wameendelea kuiomba serikali watumishi waliosalia nao walipwe na Hazina Wakurugenzi wa Halmashauri  wasimamiwe  kulipa mishahara kwa wakati kama ambavyo Hazina inavyofanya na Halmashauri hizo ni ikiwemo Geita ,Ilala, Manispaa ya Kinondoni, Mbeya Jiji,Jiji la Mwanza, Temeke manispaa, Dodoma na Morogoro.

Aidha amebainisha kuwa endapo Halmashauri hizo zitalipa mishahara ya Watumishi hao kwa wakati itaondoa ombwe kubwa lililopo katika upatikanaji wa haki na stahiki za wanachama wao 180 na kuondoa matabaka ya kiutumishi mahala pa kazai

No comments:

Post a Comment

Pages