HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 06, 2024

TPA yawa kivutio nane nane Dodoma

 

Meneja wa Uhusiano na Mawasiliano wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA)  Nicodemas Mushi (kulia) akiteta jambo na Afisa Uhusiano na Mawasiliano Mkuu wa Bandari ya Dar es salaam , Bi. Levina kato kwenye maonesho ya wakulima maarufu kwa jina Nanenane yanayoendelea kwenye viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma.

Afisa Udahili wa Chuo cha Bandari, Bi. Upendo Mfinanga (wa pili kulia ) akielezea umuhimu wa kozi mbalimbali zinazotolewa na chuo hicho kwa wageni waliotembelea Banda la Bandari kwenye maonesho ya wakulima maarufu kwa jina Nanenane yanayoendelea kwenye viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma.

Afisa Masoko wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Bi. Liliani Magesa akiwaonesha watumishi wa Kampuni ya Watumishi Housing Investment Bw. Fidelis Peterson na Bw. Obadia Erasto, fursa mbalimbali na huduma zinazotolewa na (TPA) kupitia kipeperushi, kushoto akifuatilia kwa makini ni Afisa Udahihili Bi. Upendo Mfinanga kwenye maonesho ya wakulima maarufu kwa jina Nanenane yanayoendelea kwenye viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma.

 

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

MAMLAKA ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imesema inayachukulia maonesho ya wakulima maarufu kama ‘Nane nane’  kwa uzito wa kipekee kwani mbali yakutoa fursa kwa wakulima, wafugaji, wavuvi na watanzania kujua maendeleo ya sekta ya bandari pia kuzitangaza huduma zitolewazo na mamlaka hiyo.

Akizungumza na wageni mbalimbali waliofika kwenye Banda la Bandari ndani ya viwanja vya Nanenane Nzuguni Jijini Dodoma ambako maonesho ya Nanenane yanaendelea kitaifa, Meneja Mahusiano wa Mawasiliano wa TPA, Nicodemus Mushi amesema watu wengi wamejitokeza kujionea na kujifunza shughuli mbalimbali za bandari.

“Kuna mageuzi makubwa sana yamefanyika katika sekta ya bandari hapa nchini kwani miradi mingi mikubwa imetekelezwa na mingine ipo katika utekelezwaji wa hatua mbalimbali,” amesema na kuongeza kuwa nanenane inawapa wadau, wateja na umma nafasi ya kujifunza furs ana huduma zinazotolewa.

Mushi alisema kozi mbalimbali zinazotolewa na chuo cha Bandari ni fursa ya ajira kwa vijana kwani ndiyo wanatumiwa au kuajiriwa kwenye bandari za Bahari na zile zilizopo kwenye maziwa ya Victoria, Tanganyika na Nyasa.

“Bandari imekuwa ni kiungo muhimu sana wakulima kwani bandari zetu zinatumika kusafirisha mazao kwenye masoko ya kimataifa,” alisema meneja uhusiano na mawasiliano huyo.

Aliwahimiza watanzania kuchangamkia fursa na huduma zinazotolewa na TPA pamoja na vituo vyake vilivyopo kwenye nchi mbalimbali zikiwemo Jamhuri ya Kongo, Rwanda, Zambia,Burudi, Uganda na Zimbabwe.

Kwa upande, Mkurugezi wa Kampuni inayoingiza mbolea ya Premium Agro-Chem,  Kamlesh Asawla kampuni yake ni mtumiaji mkubwa bandari kati kuingiza na kusafirisha mizigo kutoka nje ya nchi.

“Tumeshaingiza  shehena ya mbolea tani elfu kumi (10,000) inasubiri kupakuliwa. Tumekuwa wateja bandarini tangu mwaka 1994 kampuni yetu ilipoanzishwa,” alisema Asawla alisema na kuwataka watanzania wengi kujitokeza kwenye maonesho ya Nanenane Dodoma.

Alisema kufuatia umuhimu wa maonesho hayo, Kampuni ya Premium Agro-Chem inashiriki katika maonesho ilikukutana na wakulima na wakulima na mawakala wa mbolea.

No comments:

Post a Comment

Pages