HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 13, 2024

Waziri Balozi Pindi Chana afunga Onesho la 8 la Utalii la Kimataifa la Swahili, awahimiza Watanzania kutunza na kuhifadhi Rasilimali

Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam


Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Dkt. Pindi Chana amefunga Onesho la Nane la Utalii la Kimataifa la Swahili kwa kuwahimiza  Watanzania  kuzitunza na kuhifadhi rasilimali zilizopo nchini ili kuendelea kukuza Sekta ya Utalii.

Balozi Dkt Chana ametoa rai hiyo  Jijini Dar es salaam wakati akifunga Onesho la nane la Utalii la Kimataifa la Swahili ( S!TE) ambalo limefanyika kuanzia Oktoba 11 ,2024 katika Ukumbi wa Mlimani City jijini humo

Amesema kuwa utalii na ulinzi wa rasilimali za Nchi yetu ni kipaumbele cha Kila mtanzania,hivyo hakuna budi kuhakikisha kila mtanzania anafanya hivyo ili kukuza sekta ya utalii.
Amebainisha kuwa sekta ya Utalii inachangia asilimia 17 za pato la Taifa(DGP),huku ikingiza fedha za kigeni ni asilimia isiyopungua 25,ambazo ni zaidi ya Dola bilion 3.

"Tukizungumzia suala la utalii kila mtu ananufaika,kwanza shirika la ndege ATCL linapata abiria wengi wanaokuja kutalii nchini hapa,,pia mtalii anaposhuka anatumia usafiri wa ndani ambapo madereva wananufaika,hivyo hivyo ananunua bidhaa mbalimbali,hata mkulima mdogomdogo huko kijijini ananufaika kwa uuza mazao yake,huu ni  mnyororo mkubwa wa thamani katika sekta ya Utalii." Amesema 

Nakuongeza kuwa Tanzania tuna vivutio vingi ,kuna Mlima Kilimanjaro ambao ni mrefu kuliko yote Afrika Mashariki, tuna Utalii wa fukwe,mali kale, pia tuna hifadhi za National Parks zisizopungua 21, makumbusho za Taifa  zisizopungua saba.

Amesisitiza kuwa kadri siku zinavyokwenda watalii wanazidi kuongezeka ambapo kauli mbiu ya onesho la S!TE  mwaka huu " Utalii na Amani" ambapo Tanzania ni kisiwa Cha amani na imekua mfano katika nchi za Afrika Mashariki na  SDAC.

Hata hivyo Balozi Dkt. Chana ametumia fursa hiyo kuwashukuru Watanzania kwa kuendelea kudumisha amani na utilivu pamoja  na kuendeleza kudumisha mila na desturi za kitanzania  kwani imekua chachu kubwa ya kuvutia watalii.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Balozi Dkt. Ramadhan Dau amesema kuwa onesho la mwaka huu limepata mafanikio makubwa ukilinganisha nala Mwaka Jana kutokana na wanunuzi wa vifaa vya Utalii kuongezeka,makampuni ya kufanya maonesho,

"Kama alivyosema waziri,kwenye utalii kuna mambo mawili ,kwanza kuhifadhi,pili kutangaza utalii,na sisi TTB kazi yetu kubwa ni kutangaza utalii nje ya nchi na hata kwa watanzania wenyewe,lakini pamoja na hili la uhifadhi kua  lipo kwenye Wizara yetu lakini ni jukumu la kila mtanzania kuhifadhi rasilimali" amesema Balozi Dr.Dau

Nae, Kamishna Uhifadhi wa Wakala wa Misitu (TFS), Profesa Dos Santos Silayo amesema Utalii wao kwa kiasi kikubwa upo kwenye Mazingira Ikolojia ambayo ni ya kuona na kuushughulisha mwili na akili hususani kwenye masuala ya kutembea kwenye Misitu, kupumzika, kupanda milima na michezo mbalimbali.

 


No comments:

Post a Comment

Pages