Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi kesho 13 Novemba anatarajiwa kulitangaza baraza jipya la mawaziri katika hafla fupi, itakayofanyika Ikulu, Zanzibar.
Taarifa ya Ikuklu Zanzibar kwa vyombo vya habari imebainisha kuwa hafla hiyo itahudhuriwa na wahariri na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vya habari.
Katika hafla hiyo, Rais Dkt. Mwinyi anatarajiwa kuelezeawelekeo wa dira kuu ya uongozi wa baraza jipya katika kutekeleza vipaumbele vya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Vipaumbele hivyo vitajikita katika Uchumi wa Bluu, Uwekezaji, Huduma za Jamii, Miundombinu pamoja na maendeleo Jumuishi kwa Wananchi.
Sambamba na hilo Baraza la Mawaziri Wateule wataapishwa Jumamosi 15 Novemba 2025, saa nane mchana katika viwanja vya Ikulu, Zanzibar.
Taarifa hiyo inasema kuwa hafla hiyo ya uapisho ni hatua muhimu katika kuanza rasmi Kipindi cha Pili cha Serikali ya Awamu ya Nane.



No comments:
Post a Comment