KIKOSI cha Azam FC kinachonolewa na Florent Ibenge, kimeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Simba SC na kuzika jinamizi la kutopata ushindi kwenye mechi tatu mfululizo.
Azam FC walikuwa wageni kwenye dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam jioni hii, ilikoibuka na ushindi huo shukrani kwa mabao ya dakika 9 za mwisho kutoka kwa Jephte Kitambala (81) na Idd Nado (88), mabao yote yakitokana na pasi za mwisho za mtokea benchi Nassor Saadun.
Kabla ya kuivaa Simba, Azam FC ilikuwa na sare tatu mfululizo dhidi ya JKT Tanzania (bao 1-1), Namungo FC (bao 1-1) na kisha ya hivi karibuni walipoumana na Singida Black Stars na kuvuna sare tasa (0-0).
Ushindi pekee wa Kocha Ibenge raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), ulikuwa wa mabao 2-0 dhidi ya Mbeya City walioupata kwenye mechi yao ya kwanza iliyoungurumishwa kwenye dimba la Azam Complex, Chamazi.
Ushindi wa leo umeua rasmi matamanio ya baadhi ya waliokua wakitaka Suleiman Matola 'Veron' apewe mikob ya kukinoa kikosi hicho kuchukua mikoba ya Dimitar Pantev, aliyetupiwa virago hivi karibuni.





No comments:
Post a Comment