Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhajj Hemed Suleiman Abdulla amewashukuru wananchi wa Bweleo na wazanzibar kwa ujumla kwa kuendelea kuilinda amani katika kipindi chote cha uchaguzi Mkuu.
Ameyasema hayo wakati akisalimiana na waumini wa masjid TAQWA uliopo BWELEO Wilaya ya Magharibi “ B” UNGUJA mara baada ya kumalizika kwa Ibada ya swala ya Ijumaaa.
Amesema Suala la amani ni suala mtambuka linalomgusa kila mwananchi wa Zanzibar mwenye uchungu na nchi yake na anaependa kuiona zanzibar ikipiga hatua zaidi kimaendeleo.
Alhajj Hemed amefahamisha kuwa amani iliopo nchini ni urithi kutoka kwa waasisi wa Taifa hili, hivyo ni wajibu wa kila mzanzibari kuitunza na kuienzi amani iliyopo kwa maslahi mapana ya vizazi vya sasa na baadae.
Sambamba na hayo, amesema kuwa nchi yoyote duniani inategemea kuwepo kwa amani na utulivu ili kuweza kuleta maendeleo endelevu kwa wanachi wake pasipo kuangalia itikadi ya vyama vyama siasa.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amewasisitiza wananchi kuendelea kuelimishana na kuhamasisha juu ya umuhimu wa amani na utulivu katika nyanja zote za kiuchumi, kisiasa na kijamii hasa katika kipindi hiki serikali ikiendelea na ujenzi wa miradi mbali ya kimaendeleo.
Aidha, amesema Serikali iko tayari kutoa kila aina ya ushirikiano kwa wananchi wa Zanzibar na watanzania kwa ujumla ili kuhakikisha malengo ya serikali yanafikiwa kama ilivyopangwa


No comments:
Post a Comment