Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Umoja wa Wafanyabiashara Wadogo Mkoa wa Dar es Salaam umeungana kulaani vikali matukio ya uvunjifu wa amani yaliyotokea Oktoba 29,30 na 31 mwaka huu, wakieleza kuwa yalisababisha Taifa kuingia katika mgawanyiko wa kisiasa na kuathiri shughuli za kiuchumi.
Akizungumza na waandishi wa habari Desemba 24,2025 jijini Dar es Salaam, mwakilishi wa umoja huo kutoka Gongolamboto, Bakari Sufiani, amesema kuwa matukio hayo siyo desturi ya Watanzania na yameacha madhara makubwa kwa familia, wafanyabiashara na Taifa kwa ujumla.
Amesema kuwa kilichotokea kililenga kuondoa Serikali iliyokuwa madarakani kwa njia zisizo halali, jambo ambalo ni kinyume na Sheria na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Bakari ameongeza kuwa matumizi ya matusi na maneno machafu katika mitandao ya kijamii siyo njia sahihi ya kulinda amani ya Taifa, bali yanachochea chuki na kuvuruga mshikamano wa kitaifa uliodumishwa kwa miaka mingi.
Ameeleza kuwa wafanyabiashara ndani ya Jiji la Dar es Salaam walipata hasara kubwa kufuatia vurugu hizo wakati wa Uchaguzi Mkuu, na kusisitiza kuwa umoja huo unalaani vikali hali hiyo na kuomba matukio kama hayo yasijirudie tena.
Aidha, amesema kuwa baada ya vurugu za Oktoba 29, wafanyabiashara wamekuwa waathirika wakubwa huku baadhi ya watu wanaochochea vurugu wakidaiwa kuwa na uraia pacha na sehemu za kukimbilia hali inapoharibika, hivyo umoja huo unakataa aina zote za ushawishi unaolenga kuhamasisha chuki na uchochezi, pamoja na kuwakemea viongozi wa dini au mtu yeyote anayehusika na vitendo vinavyohatarisha amani ya Taifa.
Hata hivyo umoja huo umewataka Watanzania wote kujiepusha na vitendo vya vurugu vinavyoweza kuliingiza taifa katika uvunjifu wa amani, wakisisitiza kuwa machafuko hayaleti tija wala suluhu ya changamoto za kijamii na kiuchumi.
“Matukio ya Oktoba 29 yametosha kuwa somo. Tumeshuhudia athari zake na tumejifunza kuwa uvunjifu wa amani hauwezi kuleta maendeleo wala suluhu ya amani,” walisema kwa pamoja.l
Umoja huo umeeleza masikitiko yao makubwa, ukilaaani kwa nguvu zote vitendo vya uchochezi na kuwaasa vijana wa Kitanzania kutowasikiliza watu wanaohamasisha vurugu, wakiwemo baadhi ya viongozi wa ndani na wanasiasa wanaotumia fursa hizo kujinufaisha kisiasa na kwa maslahi yao binafsi.
Kwa mujibu wa tamko hilo wamesema waathirika wakubwa wa vurugu za Oktoba 29 walikuwa ni wafanyabiashara, wajasiriamali na wafanyabiashara ndogo ndogo (wamachinga), waliopata hasara kubwa kutokana na uharibifu wa mali na kusimama kwa shughuli za kiuchumi.
Kwa upande wake Mzee Omary Suleiman mfanyabiashara wa Soko la Kinondoni,akizungumza kuunga Mkono tamko hilo amesema vurugu hizo zilitokana na uchochezi wa makusudi na kusisitiza kuwa ni wajibu wa kila Mtanzania kuhakikisha matukio kama hayo hayajirudii tena.
“Tanzania ni mimi, na mimi ni nchi. Tunaomba Watanzania wote waunge mkono jitihada hizi ili Tanzania ibaki salama, yenye amani na utulivu,” alisema Mzee Suleiman.

Tamko hilo limekuja kufuatia ushirikiano wa Kituo cha Wanahabari Watetezi wa Raslimali na Taarifai (MECIRA) imeelezwa kufanya kazi kubwa ya kutoa elimu ya uraia kwa wafanyabiashara, hatua inayochangia kuongeza uelewa kuhusu haki, wajibu na umuhimu wa kulinda amani ya taifa.

No comments:
Post a Comment