HABARI MSETO (HEADER)


 


Breaking

March 05, 2026

WASIMAMIZI MIRADI YA MAENDELEO KAGERA WATAKIWA KUSIMAMIA KWA MAKINI

NA EDITHA WILLIAM, KAGERA


WASIMAMIZI wa Miradi ya Maendeleo Mkoani Kagera, wametakiwa kusimamia miradi inayotekelezwa katika maeneo yao ili kubaini changamoto zinazojitokeza wakati wa utekelezaji.



Hayo yamebainishwa Machi 4, 2026 na Mkuu wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa TAKUKURU Mkoani Kagera Bw. Vangsada Mkalimoto alipokutana na waandishi wa habari ofisini kwake wakati akielezea mafanikio ya utendaji kazi wa Taasisi hiyo kwa kipindi cha Oktoba - Disemba 2025.

Mkalimoto amesema kuwa kwa kipindi cha Oktoba-Disemba 2025 TAKUKURU imesaidia kukusanya Tsh. 57,160,177 za makusanyo ya Kodi pamoja na faini ya mizigo ya magari yaliyoingia Nchini kwa Magendo kutoka Uganda

Aidha, ameongeza kuwa Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa Wilaya ya Muleba TAKUKURU imefanikiwa kuokoa matofali 2, 830 yenye thamani ya Tsh. 7,924,000 katika mradi wa jengo la OPD katika kituo cha Afya cha Kata ya Ngenge ambayo yalibainika kuwa chini ya kiwango Cha ubora unahitajika

Kwa upande wa Wilaya ya Missenyi Taasisi hiyo kwa kushirikiana na kikosi kazi cha kuzuia Magendo tarehe 29 Disemba 2025 walifanikiwa kukamata magari matano yakiwemo maroli matatu na magari mawili ya abiria aina na hiace yakiwa yamevuka mpaka wa Tanzania na Uganda pamoja na vituo vya ukaguzi vya kyaka bila kulipa Kodi ambapo magari yote yamepatikana na kosa la uingizaji wa bidhaa Nchini bila vibali

Kwa ujumla TAKUKURU Mkoa wa Kagera imefatilia matumizi ya Tsh. 50,244,425,519.97 kwenye utekelezaji wa miradi ya maendeleo 10 ambapo miradi iliyobainika kugundulika na mapungufu ilishauriwa kufanyiwa marekebisho. 

No comments:

Post a Comment

Pages