HABARI MSETO (HEADER)


 


Breaking

March 20, 2026

Jeshi la Polisi Kagera latoa onyo kali kwa waendesha vyombo vya moto wakati wa sikukuu

NA EDITHA WILLIAM, BUKOBA KAGERA


Jeshi la Polisi Mkoa wa Kagera limetoa onyo kwa waendesha vyombo vya moto kuepuka kuendesha wakiwa wamelewa katika kipindi cha sikukuu za IDD na Pasaka, likisisitiza kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa yeyote atakayebainika kufanya hivyo.

Onyo hilo limetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Blasius Chatanda, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake. Amesema lengo ni kupunguza ajali na kulinda usalama wa wananchi katika kipindi hiki cha sherehe.


Aidha, Kamanda Chatanda amewataka wazazi na walezi kuhakikisha hawawaachi watoto kwenda peke yao barabarani au katika maeneo ya fukwe wakati wa sikukuu, ili kuepuka ajali na matukio ya vifo yanayoweza kujitokeza.


“Fukwe ni sehemu ambazo watu wengi hupendelea kwenda kufurahi na familia zao.


 Natoa rai kwa wazazi kuhakikisha watoto hawaendi peke yao, bali waambatane na watu wazima, kwani ni rahisi kwa mtu mzima kutoa msaada pale panapotokea hatari, hasa wakati wa kuogelea,” alisema.


Pia amekemea tabia ya kuendesha vyombo vya moto wakiwa wamelewa, akieleza kuwa hali hiyo hupunguza umakini barabarani na kuongeza hatari ya ajali, hususan kwa watoto ambao mara nyingi hawana uelewa wa kutosha wa sheria za usalama barabarani.


Amesisitiza kuwa uzembe huo unaweza kusababisha vifo au majeruhi. 



No comments:

Post a Comment

Pages