HABARI MSETO (HEADER)


 


Breaking

June 22, 2026

CLEAN COOKING MARATHON KURINDIMA DAR JUNI 27

JUMUIYA ya Wafanyabiashara Wanawake Tanzania @tabwa_tz (TABWA), kwa kushirikiana na Wizara ya Nishati,hii leo imetoa ratiba na maandalizi ya matukio makuu mawili yenye lengo la kuleta mapinduzi ya matumizi ya nishati safi ya kupikia nchini. 



Matukio haya yanaongozwa na kauli mbiu: “Tumia Nishati Safi: Linda Mazingira, Tunza Afya, Okoa Muda kwa Uchumi Endelevu.

Tukio la kwanza ni Kongamano na Maonesho ya Tatu yatafanyika rasmi kuanzia tarehe 23 hadi 25 Juni 2026 katika ukumbi wa East Africa Logistics Centre (EACLC) uliopo Ubungo, Dar es Salaam.

Huku Tukio la pili ni siku ya Jumamosi, tarehe 27 Juni 2026, kupitia mbio za @cleancookingmarathon Clean Cooking Marathon msimu wa pili zitakazofanyika katika viwanja vya St. Peters Oysterbay, Dar es Salaam. Mbio zitahusisha kilomita 21, 10, na 5,ambapo uzinduzi wa jezi za tukio hilo umefanyika hii leo.

Lengo kuu la Marathon hii ni Kuchangisha Fedha (Fundraising) kwa ajili ya kuendesha mafunzo endelevu katika mikoa 10 ya kimkakati ya Tanzania. Mikoa hiyo ni pamoja na: ● Dar es Salaam, Pwani, na Arusha (ambayo tayari mafunzo yameshafanyika). ● Dodoma, Kilimanjaro, Mbeya, Shinyanga, Mwanza, Mtwara, na Tabora (itakayofikiwa ndani ya muda uliopangwa).

Siku hiyo ya tarehe 27 Juni, kutakuwa na tamasha la kipekee la "Bata la Nishati Safi ya Kupikia", ambapo kutakuwa na burudani na mapishi ya mubashara kwa kutumia  mkaa mbadala na majiko ya gesI, ili kuonyesha kivitendo ladha na usalama wa nishati safi

 Kwa Mawasiliano na Maelezo Zaidi: Simu: 0758 664 664


No comments:

Post a Comment

Pages