Na Hellen Ngoromera
BODI ya Bima ya Amana nchini (DIB) imeanzisha utaratibu mpya wa kuzipunguzia hasara benki zinazoingia kwenye migogoro au changamoto za kiuendeshaji.
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano ya Umma wa bosi hiyo Lwaga Mwambande amesema hayo Julai 6 Jijini Dar es Salaam katika Maonyesho ya Jubilei ya dhahabu ya miaka 50 ya Sabasaba yanayoendelea katila viwanja vya Sabasaba.
Amesema badala ya kusubiri mpaka benki ife ndipo bodi yake ilipe fidia wameona ianzishe utaratibu huo ambao ni mzuri na wenye manufaa makubwa.
"Badala ya kusubiri mpaka benki ife ndipo tulipe fidia sasa tuna jukumu la kupunguza hasara kwa benki zinazopita changamoto hizo," amesema Lwaga.
Ameeleza kwamba utaratibu huo umeanza katika mwaka mpya wa fedha ulioanza Julai na kwamba Benki Kuu ya Tanzania(BoT) ndiyo yenye jukumu la kushughulikia jambo hilo. Hata hivyo ameweka wazi kwamba hadi sasa hakuna benki iliyofikia katika hali hiyo.
"Mpango huo ni mzuri na wenye manufaa kwani ni nafuu kuliko kulipia fidia. "Wataalamu wanasema kupunguza hasara wakati mwingine ni nafuu kuliko kulipa fidia, unaweza kukuta benki inahitaji Shs.mlioni 500 ili irejee kwenye utendeji wa kawaida na mkiiacha ikafa mnaweka mkakuta fidia inakuwa hadi milioni 2," amesema Lwaga.
Amebainisha kuwa katika vitu ambavyo bodi hiyo inajitahidi ni kuwa mwangalifu katika mfuko wa amana.
Bodi ya amana imeanzishwa kwa lengo la kukinga amana za wananchi katika benki na taasisi za kifedha na inapotokea benki ambazo wananchi hao wanaweka fedha zao zinafilisika amana zao zingawiwa kikamilifu.





No comments:
Post a Comment