HABARI MSETO (HEADER)


 


Breaking

August 06, 2026

Waziri Kombo aagana na Balozi wa Ufaransa

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mheshimiwa Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.) amemuaga Balozi wa Ufaransa anayemaliza muda wa uwakilishi nchini, Mheshimiwa Anne-Siphie Avé jijini Dar Es Salaam Agosti 4, 2026.


Wakati wa mazungumzo hayo Mheshimiwa Waziri Kombo amemshukuru na kumpongeza Balozi Avé kwa kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia baina ya Ufaransa na Tanzania katika kipindi chake cha uwakilishi.



Katika kipindi cha uwakilishi wake, Balozi Avé alikuwa mstari wa mbele katika kukuza Utamaduni, Sanaa na Michezo nchini kwa kushiriki na kuandaa shughuli mbalimba ikiwemo Mashindano ya Ubunifu wa Khanga, Mashindado ya Wapiga picha za michezo na kadhalika.



Kwa upande wake, Balozi Avé alimshukuru Balozi Kombo na Serikali kwa ujumla kwa kumpatia ushirikiano uliomuwezesha kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi. Aidha, alimpongeza Waziri Kombo kwa kazi kubwa anayoifanya ya kusimamia diplomasia ya nchi na kuahidi kuwa atakuwa Balozi mzuri wa kutangaza uzuri wa Tanzania ikiwemo fursa za uwekezaji na utalii.



No comments:

Post a Comment

Pages