Na Elizabeth John
NYOTA wa filamu nchini, Jacline Wolper anajipanga
kusambaza kazi yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Princess’, hivi karibuni.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Wolper alisema
yupo katika hatua za mwisho za uandaaji wa kazi hiyo ambayo anamini itakuwa
gumzo mtaani kutokana na stori ambayo ameielezea ndani yake.
Alisema anawaomba wadau wa kazi zake wakae mkao wa kula
kwaajili ya kazi hiyo ambayo anatarajia kuisambaza hivi karibuni.
“Namshukuru mungu maandalizi ya kazi yangu yameenda
vizuri na hadi sasa ndio namalizia kazi hii, wapenzi wa kazi zangu wake vizuri
kwaajili ya kuipokea kazi hii ambayo imefuata maadili ya mtoto wa kitanzania,”
alisema Wolper.
Alisema yeye ni Mtanzania hivyo ameamua kufanya kitu
ambacho kipo katika jamii inayomzunguka na kuelimisha kwa uwezo aliokuwa nao
yeye.
No comments:
Post a Comment