HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 10, 2013

ARSENE WENGER ATAKA WACHEZAJI SOKA WAPIMWE DAMU


LONDON, England

Kauli ya Wenger inakuja kufuatia daktari wa Kihispania Eufemiano Fuentes kufichua kuwa amekuwa na orodha ya wateja wanasoka wanaotumia dawa haramu kama ilivyo kwa waendesha baiskeli wenye kesi juu ya sakata hilo

MFARANSA anayaeinoa Arsenal, Arsene Wenger, ameshauri kuwe na vipimo vya damu kwa wachezaji wa soka na sio mkojo pekee, ili kuondoa tatizo la udanganyifu na matumizi ya dawa zilizopigwa marufuku michezoni.

Wenger amesisitiza umuhimu wa kutumia damu badala ya mkojo, ambapo alisema: “Maofisa wa Kudhibiti Dawa Haramu wa UEFA hawachukui sampuli za damu, wao wanachukua mkojo pekee. Nimeuiliza juu ya hilo mara nyingi, kuna haja ya kubadilika.

“Mara nyingine unaweza kusubiri hadi kwa masaa mawili baada ya mechi kumalizika, hivyo kama watachukua vipimo kwa sampuli za damu inaweza kuleta wepesi na uharaka.

“Natumaini hatuna tatizo kubwa katika utumiaji wa dawa haramu, lakini tutajaribu kujiangalia katika hilo na kuona ni kwa namna gani tunaweza kuingia katika udhibiti.

“UEFA wako tayari kufanya hivyo, lakini unaleta matatizo ya kimaadili na kitabibu kwa sababu kila mmoja anaweza kukubali kupimwa damu na si kila mtu yuko tayari kufanya uchunguzi wa aina hiyo.”

Kauli ya Wenger inakuja kufuatia daktari wa Kihispania Eufemiano Fuentes kufichua kuwa amekuwa na orodha ya wateja wanasoka wanaotumia dawa haramu kama ilivyo kwa waendesha baiskeli wenye kesi juu ya sakata hilo.

……The Sun……

No comments:

Post a Comment

Pages