Rafael Nadal akirudisha mpira kwa mpinzani wake Daniel Gimenyo-Traver (hayupo pichani) wakati wa mechi ya robo fainali ya michuano ya Chile Open 2013 jana.
SANTIAGO,
Chile
Chile Open 2013 ni
michuano ya kwanza kwa Nadal, bingwa mara 11 wa Grand Slam tangu mwaka 2012
aliouanza na kuumaliza akikosa mikubwa
NYOTA wa tenisi duniani, Rafael Nadal amefanikiwa kutinga
nusu fainali ya michuano ya Wazi ya Chile ‘Chile Open 2013’
inayoendelea jijini hapa na kuendeleza moto wa mafanikio wakati huu anaorejea
kutoka katika majeraha ya muda mrefu.
Kinara huyo wa zamani wa viwango vya ubora vya mchezo huo
duniani, ambaye alikuwa nje ya uwanja kwa miezi saba akiuguza jeraha la goti,
amefanikiwa kumchapa Mhispania mwenzake Daniel Gimeno-Traver kwa 6-1 6-4 na
kutinga hatua hiyo.
Nadal, 26, jana alikuwa akisubiria pambano la robo faniali
nyingine kutambua ataumana na nani katika nusu fainali itakayopigwa leo
Jumapili. Mpinzani wake alitarajiwa kupatikana katika mechui kati ya Mfaransa
Jeremy Chardy au Mtaliano Paolo Lorenzi.
Chile
Open 2013 ni michuano ya kwanza kwa Nadal, bingwa mara 11 wa Grand Slam tangu
mwaka 2012 aliouanza na kuumaliza akikosa mikubwa.
Nadal alikosa michuano ya Olimpiki ya Majira ya Joto,
iliyofanyika jijini London
mwaka jana kutokana na matatizo ya goti, yaliyomuondoa pia katika michuano ya
wazi ya Marekani ‘US Open’.
……BBC……
No comments:
Post a Comment