LONDON,
England
Kauli ya Wenger
inakuja kufuatia daktari wa Kihispania Eufemiano Fuentes kufichua kuwa amekuwa
na orodha ya wateja wanasoka wanaotumia dawa haramu kama ilivyo kwa waendesha
baiskeli wenye kesi juu ya sakata hilo
MFARANSA anayaeinoa Arsenal, Arsene Wenger, ameshauri kuwe
na vipimo vya damu kwa wachezaji wa soka na sio mkojo pekee, ili kuondoa tatizo
la udanganyifu na matumizi ya dawa zilizopigwa marufuku michezoni.
Wenger amesisitiza umuhimu wa kutumia damu badala ya mkojo,
ambapo alisema: “Maofisa wa Kudhibiti Dawa Haramu wa UEFA hawachukui sampuli za
damu, wao wanachukua mkojo pekee. Nimeuiliza juu ya hilo mara nyingi, kuna haja ya kubadilika.
“Mara nyingine unaweza kusubiri hadi kwa masaa mawili baada
ya mechi kumalizika, hivyo kama watachukua
vipimo kwa sampuli za damu inaweza kuleta wepesi na uharaka.
“Natumaini hatuna tatizo kubwa katika utumiaji wa dawa
haramu, lakini tutajaribu kujiangalia katika hilo na kuona ni kwa namna gani tunaweza
kuingia katika udhibiti.
“UEFA wako tayari kufanya hivyo, lakini unaleta matatizo ya
kimaadili na kitabibu kwa sababu kila mmoja anaweza kukubali kupimwa damu na si
kila mtu yuko tayari kufanya uchunguzi wa aina hiyo.”
Kauli ya Wenger inakuja kufuatia daktari wa Kihispania Eufemiano
Fuentes kufichua kuwa amekuwa na orodha ya wateja wanasoka wanaotumia dawa
haramu kama ilivyo kwa waendesha baiskeli wenye kesi juu ya sakata hilo.
……The Sun……
No comments:
Post a Comment