HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 27, 2013

ASNATH NDIYE REDD'S MISS HIGHER LEARNING MOROGORO 2013

 Redd’s Miss Higher Learning Mkoa wa Morogoro, Asnath Mwakitwange (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na mshindi wa pili Rosemary Aloyce (kulia) na Mshindi wa tatu Tarchisic Mtui, mara baada ya warembo hao kutawazwa kuwa washindi wa Shindano hilo usiku wa kuamkia leo katika shindano lililofanyika Mjini Morogoro. Anitha ambaye ni Mwanafunzi wa Chuo Kikuu Mzumbe, aliwashinda warembo wenzake 10 aliokuwa akiwania nao taji hilo. (Picha zote na Mpiga Picha Wetu)
 Mshindi wa Shindano la Redd’s Miss Higher Learning Mkoa wa Morogoro, Asnath Mwakitwange kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe akipunga mkono mara baada ya kuvikwa taji hilo usiku wa kuamkia jana Mjini Morogoro. 
 Warembo waliofanikiwa kuingia Tano Bora ya Redd’s Miss Higher Learning Mkoa wa Morogoro wakiwa katika picha ya pamoja, kutoka kushoto ni Tarchisic Mtui, Rosmary Aloyce, Hellen Mhando, Tausi Idd na Asnath Mwakitwange aliyeibuka mshindi.
 Washiriki wa shindano la  Redd’s Miss Higher Learning Mkoa wa Morogoro wakicheza show ya ufunguzi wa shindano hilo lililofanyika usiku wa kuamkia leo na kushirikisha warembo 11 kutoka vyuo mbalimbali vya Elimu ya Juu mkoani humo.
Mshindi wa tatu wa kinyang'anyiro hicho, Tarchisic Mtui akizungumza machache akiwa na vazi la ubunifu lilitengenezwa kwa kutumia majani ya mti wa Muashoki.
Mshiriki Hellen Mhando akipozi kwa picha akiwa na vazi la ufukweni.
Redd’s Miss Higher Learning mkoa wa Morogoro, Asnath Mwakitwange, akijinadi mbele ya majaji na kivazi cha ufukweni 
 Mshiriki wa shindano la kumsaka Redd’s Miss Higher Learning mkoa wa Morogoro, Hellen Mhando akipita jukwaani kujinadi mbele ya majaji na kivazi cha usiku. 
Mkali wa muziki wa kizazi kipya Tanzania ‘Bongo Fleva,’ Barnaba Boy akitumbuiza mashabiki wa tasnia ya urembo wakati wa shindano la kumsaka Redd’s Miss Higher Learning Mkoa wa Morogoro jana usiku. 

No comments:

Post a Comment

Pages