Redd’s Miss Higher Learning Mkoa wa Morogoro,
Asnath Mwakitwange (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na mshindi wa pili
Rosemary Aloyce (kulia) na Mshindi wa tatu Tarchisic Mtui, mara baada ya warembo
hao kutawazwa kuwa washindi wa Shindano hilo usiku wa kuamkia leo katika
shindano lililofanyika Mjini Morogoro. Anitha ambaye ni Mwanafunzi wa Chuo
Kikuu Mzumbe, aliwashinda warembo wenzake 10 aliokuwa akiwania nao taji hilo . (Picha zote na Mpiga Picha Wetu)
Mshindi wa Shindano la Redd’s Miss Higher
Learning Mkoa wa Morogoro, Asnath Mwakitwange kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe
akipunga mkono mara baada ya kuvikwa taji hilo usiku wa kuamkia jana Mjini Morogoro.
Warembo waliofanikiwa kuingia Tano Bora
ya Redd’s Miss Higher Learning Mkoa wa Morogoro wakiwa katika picha ya pamoja, kutoka kushoto ni Tarchisic Mtui, Rosmary Aloyce, Hellen Mhando, Tausi Idd na
Asnath Mwakitwange aliyeibuka mshindi.
Washiriki wa shindano la Redd’s Miss Higher Learning Mkoa wa Morogoro
wakicheza show ya ufunguzi wa shindano hilo
lililofanyika usiku wa kuamkia leo na kushirikisha warembo 11 kutoka vyuo
mbalimbali vya Elimu ya Juu mkoani humo.
Mshindi wa tatu wa kinyang'anyiro hicho, Tarchisic Mtui akizungumza machache akiwa na vazi la ubunifu lilitengenezwa kwa kutumia majani ya mti wa Muashoki.
Mshiriki Hellen Mhando akipozi kwa picha akiwa na vazi la ufukweni.
Redd’s Miss
Higher Learning mkoa wa Morogoro, Asnath Mwakitwange, akijinadi mbele ya majaji
na kivazi cha ufukweni
Mshiriki wa shindano la kumsaka Redd’s Miss
Higher Learning mkoa wa Morogoro, Hellen Mhando akipita jukwaani kujinadi mbele
ya majaji na kivazi cha usiku.
Mkali wa muziki wa kizazi kipya Tanzania ‘Bongo Fleva,’
Barnaba Boy akitumbuiza mashabiki wa tasnia ya urembo wakati wa shindano la
kumsaka Redd’s Miss Higher Learning Mkoa wa Morogoro jana usiku.
No comments:
Post a Comment