HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 27, 2013

MAONYESHO YA UOKOAJI NA WAJASIRIAMALI YALIOANDALIWA NA MAMLAKA YA USALAMA MAHALA PA KAZI OSHA JIJINI ARUSHA



Wafanyakazi wa kampuni Afrikan barrik wakiwaonyesha wananchi jinsi ya okoaji wakiwa kwenye maeneo yao ya kazi migodini kwenye maonyesho yanayoendelea kwenye viwanja vya sheikh Amri Kaluta Abeid jijini Arusha kwa siku Tatu yakiwa ni mwengelezo wa warsha ya mamlaka ya usalama mahala pa kazi(OSHA)picha na mahmoud ahmad arusha.
Picha juu na chini ni  Mratibu wa uokoaji kwenye migodi kutoka kampuni ya Noth Mara Poul Kagondi akiwa na Damian Adrea kushoto na kulia ni mratibu mkuu wa usalama wa afya kazini kwenye mgodi wa Noth Mara Aggrey Kileo wakiwa wanawaeleza jinsi ya uokoaji kwenye mgodi wao. (Picha na Mahmoud Ahmad Arusha)
Banda la wauzaji wa dawa kutoka china kampuni ya TIENS ambao nao walishiriki katika maonyesho yaliondaliwa na mamlaka ya usalama mahala pa kazi OSHA wakionyesha bidhaa wanazouza kwenye maonyesho hayo huku wakiwataka wananchi wafike ofisini kwao jengo la KKKT jijini hapa kupata bidhaa zao na pichani ni muuzaji wa dawa hizo bi Beatrice Kiimbi kama alivyokutwa na kamera yetu kwenye uwanja wa sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
George Alando meneja usalama na afya wa kampuni ya Layne Driling ya jijini Morogoro akiwa na mwenzake kwenye banda lao wakati wa maonyesho ya usalama mahala pa kazi yanayoendelea jijini Arusha na yatafunguliwa na waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mizengo Peter Pinda siku ya jumapili ambayo itakuwa ni siku ya ukoaji mahala pa kazi
Dada devothar posta mratibu wa uokoaji kwenye mgodi wa Tulawaka akiwa na Alex kasengo mkuu wa usalama mahala pa kazi na elasto emanuel wakitoa maelezo kwenye banda la kampuni hiyo kwenye maonyesho ya usalama mahala pa kazi jijini Arusha 

No comments:

Post a Comment

Pages