Na Elizabeth John
BAADA ya kutamba na ngoma yake ya ‘Kitumbua’, mkali wa
muziki wa mduara nchini, Ally Ramadhan 'AT' anatarajia kuachia kazi mpya
inayokwenda kwa jina la ‘Anapenda’.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, nyota huyo alisema
kazi hiyo anatarajia kuisambaza katika vituo mbalimbali vya radio baada ya
kukamilika.
“Nashukuru Mungu kupata nafasi nyingine tena ya kurudi
katika kazi yangu baada ya kimya kisichojulikana," alisema.
Msanii huyo ambaye anajulikana kama mfalume wa muziki huo
kwa sasa alifanya vizuri na vibao mbalimbali kikiwemo Kifuu Tundu, Bao la Kate
na nyinginezo ambazo zilimpa umaarufu mkubwa katika tasnia ya muziki huo.
Pia mkali huyo yuko katika hatua za mwisho kukamilisha video
ya kazi yake inayoitwa ‘Kitumbua’, ambayo muda wote itaanza kuonekana kupitia
kwenye runinga runinga na akiamini utapata nafasi kubwa ya kuwakonga mashabiki
wa tasnia hiyo.
Hivyo, aliwaomba mashabiki kumuunga mkono katika kazi zake
zijazo ili kuhakikisha anafikia malengo aliyojiwekea katika tasnia hiyo ya
muziki wa kizazi kipya nchini hususan wa ‘Mduara’ ambao anaendelea kufanya
vizuri na kutishia waliopo kwenye burudani hiyo.
No comments:
Post a Comment