HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 28, 2013

STAMINA KUTOKA NA DARASA


 Na Elizabeth John

MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini, Boniventure Kabobo ‘Stamina’ anatarajiwa kuachia wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la ‘Mwambie mwinzio’ hivi karibuni.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Stamina alisema katika wimbo huo ameshirikiana vizuri na mkali wa hip hop nchini, Darasa,  na anaimani kuwa, utafanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio.

“Nashukuru nyimbo zangu kukubalika na wadau mbalimbali, ambao wananipa msukumo wa kutunga mashairi yangu kwa utulivu na umakini mkubwa, hivyo wakae tayari kwa ajili ya kuipokea ngoma hiyo,” alisema Stamina.

Msanii huyo alishafanya nyimbo kadhaa ambazo zinaendelea kufanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio na runinga zikiwemo ‘Alisema’ ‘Ushauri Nasaha’ na ‘Kabwela’.

Pia alisema yupo katika hatua za mwisho za uandaaji wa video ya kazi hiyo ambayo anaamini ataipeleka sokoni pamoja na video yake ili kuwapa burudani kamili mashabiki wake.




No comments:

Post a Comment

Pages