HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 30, 2014

LINEX: SIGOMBEI UBUNGE 2020

NA ELIZABETH JOHN

MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini, Sunday Mangu ‘Linex’ amesema ameghairi kugombea ubunge mwaka 2020 kama alivyokuwa amepanga kutokana na kuona kwamba mashabiki wake bado wanamhitaji katika sanaa.

Linex alishawahi kutamba na ngoma zake kama Mahakama ya Mapenzi, Aifola, Unataka Ndoa au Harusi na nyinginezo ambazo zilimtambulisha na kufanya vizuri katika tasnia hiyo.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Linex alisema, awali baada ya kutangaza hivyo alipata maswali mengi sana kutoka kwa mashabiki wake, hivyo ameamua kuendelea na muziki kwanza.

“Ni vizuri tukiwa na ndoto za baadae katika maisha yetu, ndoto ya kugombea ubunge ipo lakini sio 2020 kwasasa naona niendelee na muziki kwasababu nimegundua kwamba wadau bado wananitaka,” alisema Linex.

Linex aliwataka wadau wa kazi zake waendelee kumapa sapoti katika muziki wake na kwamba yupo katika mikakati ya kusambaza ngoma yake mpya ambayo bado hajaipatia jina na kwamba katika wimbo huo kuna sehemu itasikika sauti ya  Mbunge wa Kigoma, Zitto Kabwe.

No comments:

Post a Comment

Pages