HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 30, 2014

CHIDI BENZI AMFUNDA DIAMOND PLATINUMZ



NA ELIZABETH JOHN
Chidi Benzi
MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini, Rashid Makwilo Chidi Benzi’ amemshauri nyota wa muziki huo, Diamond Platinumz asitumie madawa ya kulevya, sigara wala pombe ili kuendelea kung’ara katika tasnia hiyo.
Diamond Platinumz
Akihojiwa katika kipindi cha XXL kinachorushwa na Clouds, Chidi Benzi alisema, ameamua kumshauri kama mdogo wake na pia anapenda kazi zake hataki kumpoteza mapema katika tasnia hiyo.

Chidi alisema, aliwahi kufanya kazi na Diamond kama mdogo wake hapo zamani wakati Dimond anaanza muziki na alimwambia kwamba hatumii vitu hivyo amemtaka aendelee hivyo.

“Diamond ni mdogo wangu sana, nilishirikiana naye katika wimbo wake wa ‘Nalia’ wakati ndio anaanza, na juzi kanisaidia sana katika wimbo wangu mpya kagharamia kila kitu pia kanihaidi kugharamia video ya wimbo huo,” alisema.

Aidha, Chid ametambulisha ngoma yake mpya inayojulikana kwa jina la ‘Mpaka kuchee’ ambayo ameshirikina na nyota wa muziki huo, Diamond, AY na Dully Sykes.

Alisema wimbo huo umetengenezwa na watayarishaji wa muziki huo kutoka studio za Nyumba ya Kukuza Vipaji Tanzania (THT), Emma The Boy na Tuddy Thomas.

No comments:

Post a Comment

Pages