HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 30, 2014

PRODUCER GQ:Nina ndoto kufanya kazi nawasanii wakubwa wakiwemo Chid Benz,Juma Nature,C Pwaa na Prof Jay.



NA SYLVESTER DAVID

MWANDAAJI chipukizi wa muziki wa kizazi kipya nchini kutoka katika studio za Digital Vibe mjini Morogoro, Fabian Venance maarufu kama ‘Gq’ amesema kuwa ndoto yake kubwa ni kufanya kazi na mastaa kibao nchini ili kuimarisha soko kwa mashabiki wake.
 
Akizungumza kwa njia ya simu  na Tanzania Daima jana kutoka Morogoro alisema yupo kwenye mchakato wa makubaliano ya kufanya kazi na wasanii wakubwa wakiwemo Chid Benz,Juma Nature,C Pwaa na Prof Jay. 
 
“Nimeshafanya kazi na wasanii wengi nchini na huu ni muda na kutimiza ndoto zangu za kufanya kazi na mastaa wakubwa ili kudhihirisha uwezo wangu wa kuandaa muziki mzuri na unaotakiwa na mashabiki wangu”.Alisema Gq
 
Gq alisema kuwa amefanya kazi mbili za Afande Selle ambazo zimefanya vizuri katika vyombo mbalimbali vya habari nchini ambazo ni Amani na upendo aliyomshirikisha Mc Koba pamoja na Dini Tumeletewa aliyomshirikisha Belle 9 pia alishafanya kazi na wasanii wakubwa kama Stamina na Godzilla.
 
Vilevile aliongeza kuwa mashabiki wa muziki wake wakae tayari kwa ajili ya mapokezi ya kzai kibao kutoka kwake na Studio ya Digital Vibe kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment

Pages