HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 05, 2015

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA PILI WA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII

Makamu wa Rais Dk. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na waandishi wa habari mara baada kufungua Mkutano Mkuu wa Pili wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii uliofanyika jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mratibu wa mkutano huo, Ofisa Mtendaji wa MN Capital Group, Michael Ndinisa. (Picha na Francis Dande)


Na Mwandishi Wetu

MAKAMU wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, amesema serikali itahakikisha kila mstaafu analipwa mafao yake kutoka katika  Mifuko yao ya  Hifadhi ya Kijamii.

Bilal, alisema hayo jijini Dar es Salaam leo, wakati akizindua Mkutano wa Pili wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii likiongozwa na Mamlaka ya Udhiti wa Usalama wa Mifuko hiyo (SSRA).

Alisema hivyo, kwa vile serikali inatambua kazi nzuri iliyofanywa na wastaafu ambao wengi wao walifanya kazi kwa uaminifu mkubwa na hatimaye kuchangia maendeleo  nchini hii.

Alisema, kuchangia kwao maendeleo ya nchi, kumetokana na wao kuchngia fedha nyingi katika mifuko hiyo, wakati walipokuwa bado wajiriwa katika Idara na Sekta mbalimbali za serikkali.

“Mifuko hii tumeianzisha makusudi ili kuwalea wastaafu baada ya kuwa wamefanya kazi nzuri katika nchi yetu hivyo hawastahili kuachwa wahangaike,”alisema Dk. Bilal.

Aidha, Dk. Bilal aliwataka wasimamizi wa mifuko hiyo kutumia mkutano huo kama chachu itakayozidi kuwajengea uwezo wa kuelewa maeneo mbalimbali uwekezaji.

“Hivi sasa mifuko huo inawekeza kwa ajili ya kujitunisha na lengo kubwa ikilenga kuwasaidia wanachama wake katika masuala mbalimbali ya kijamii ikiwemo ajira,”alisema Dk. Bilal.

Mkaguzi Mkuu wa Mifuko ya Ndani (SSRA), Piter Mberwa, alisema kuwa hivi sasa imetoa muongozo ambao utatumika kisheria na mifuko hiyo ikilinganishwa na awali ilipokuwa ikikabiliwa na changamoto ya ukosefu wa sheria.

Alisema muongozo huo utaendelea kuweka mazingira bora yatakayopanua wigo wa hifadhi ya jamii ikiwemo kuongeza wanachama hususan kwenye Sekta isiyo rasmi.

Kongamano hilo la mifuko ya kijamii zaidi ya 20 ya ndani linaendelea tena leo katika Ukumbi wa Serena jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Pages