Makamu wa Rais Dk. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na
waandishi wa habari mara baada kufungua Mkutano Mkuu wa Pili wa Mifuko ya
Hifadhi ya Jamii uliofanyika jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mratibu wa mkutano huo, Ofisa Mtendaji wa MN Capital Group, Michael Ndinisa. (Picha na Francis
Dande)
Na Mwandishi Wetu
MAKAMU wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, amesema serikali
itahakikisha kila mstaafu analipwa mafao yake kutoka katika Mifuko yao ya Hifadhi ya Kijamii.
Bilal, alisema hayo jijini Dar es Salaam leo, wakati akizindua
Mkutano wa Pili wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii likiongozwa na Mamlaka ya Udhiti
wa Usalama wa Mifuko hiyo (SSRA).
Alisema hivyo, kwa vile serikali inatambua kazi nzuri iliyofanywa na
wastaafu ambao wengi wao walifanya kazi kwa uaminifu mkubwa na hatimaye
kuchangia maendeleo nchini hii.
Alisema, kuchangia kwao maendeleo ya nchi, kumetokana na wao kuchngia
fedha nyingi katika mifuko hiyo, wakati walipokuwa bado wajiriwa katika Idara
na Sekta mbalimbali za serikkali.
“Mifuko hii tumeianzisha makusudi ili kuwalea wastaafu baada ya kuwa
wamefanya kazi nzuri katika nchi yetu hivyo hawastahili kuachwa
wahangaike,”alisema Dk. Bilal.
Aidha, Dk. Bilal aliwataka wasimamizi wa mifuko hiyo kutumia mkutano
huo kama chachu itakayozidi kuwajengea uwezo wa kuelewa maeneo mbalimbali uwekezaji.
“Hivi sasa mifuko huo inawekeza kwa ajili ya kujitunisha na lengo
kubwa ikilenga kuwasaidia wanachama wake katika masuala mbalimbali ya kijamii
ikiwemo ajira,”alisema Dk. Bilal.
Mkaguzi Mkuu wa Mifuko ya Ndani (SSRA), Piter Mberwa, alisema kuwa
hivi sasa imetoa muongozo ambao utatumika kisheria na mifuko hiyo
ikilinganishwa na awali ilipokuwa ikikabiliwa na changamoto ya ukosefu wa
sheria.
Alisema muongozo huo utaendelea kuweka mazingira bora yatakayopanua
wigo wa hifadhi ya jamii ikiwemo kuongeza wanachama hususan kwenye Sekta isiyo
rasmi.
Kongamano hilo la mifuko ya kijamii zaidi ya 20 ya ndani linaendelea
tena leo katika Ukumbi wa Serena jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment