HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 23, 2016

KAMPENI YA KUPIGA VITA NDOA NA MIMBA ZA UTOTONI YA BINTI WA KITAA YAFANYIKA TABATA JIJINI DAR

Bibi Pili Abdallah akielezea kwa kina maisha ya Mabinti wadogo yanayowapelekea kupata Mimba za utotoni na kuolewa wakiwa wadogo, pia alizungumzia Tamaa na Matamanio yalivyo na nguvu ya kuwafanya watoto wakike kujiingiza katika maswala ya ngono wakiwa wadogo na kupelekea kupata mimba, mwisho aliwashauri wazazi wenzake kuwatambua watoto  wao.
 Mwenyekiti  wa Serikali ya Mtaa wa Tenge Athuman Mpwenewe akieleza namna ambavyo kumekuwa na Mimba nyingi za utotoni katika mtaa wake na juhudi ambazo zimefanywa na  Serikali ya Mtaa kuhakikisha swala hilo linatokomezwa kabisa na mwisho alizungumzia vikao na wanamtaa  vinavyosaidia kutatua tatizo hilo.
Mwanaharakati Kijana Victoria Mwanziva akijibu swali na kuelezea kwa kina tafsiri ya Jinsia.
 Bi. Mwama Ajabu akielezea namna Simu zilivyoweza kuwaharibu watoto wa kike na kuongeza kuwa wazazi hawana muda nao ndio mana hizo simu zimawaharibu sana, na mara nyingi hufanya mawasiliano kisiri mida ya usiku wakati watu wamelala na kibaya zaidi watoto hao hupendelea zaidi kufatilia mitandao ambayo sio mizuri, ameshauri wazazi mwenzake kuwa lazima wawe karibu na mabinti zao.
 Baadhi ya wahusika wa Binti Kitaa wakiongea na Bodaboda waliofika katika kampeni ya Binti wa Kitaa
 Anna akizungumzia Jinsi Binti wa Kitaa inavyofanya kazi.
Mhandisi Eliwanjeria James  kutoka Kikundi cha Mainjinia wanawake Tanzania akielezea kwa kina juu ya kampeni ya Binti wa Kitaa.
 Mkurugenzi Mtendaji wa (CVF) Ndg. George David maarufu kwa  Ambassador Angelo akiendela kutoa Mwongozo.
Mwakilishi wa  Sunshine Group akipokea Cheti cha Shukurani kutoka kwa Binti wa Kitaa.
Mwakilishi kutoka GW Health World Limited akipokea Cheti cha Shukurani kutoka Binti wa Kitaa.
Aliyemwakilisha Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Tabata  Sajenti Geoffrey Kapenejele ambaye pia yupo katika Dawati akielezea namna wanavyotoa elimu kuhusiana na Jinsia katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na Mashuleni pia kwa madereva Bodaboda ambao wamekuwa wakilalamikiwa  kusababisha Mimba nyingi za utotoni, Mwisho aliomba jamii kwa ujumla kushirikiana ili kupiga vita swala hilo.
Mambinti wakiwa katika Kampeni ya Binti wa Kitaa
Mwakilishi wa Sunshine Group Fatuma akielezea namna mimba za utotoni zinavyo athiri maisha ya Binti na pia kusababisha matatizo ya kiafya na kumsababisha akose mambo mengi na kuahidi kuendelea kushirikiana na kampeni ya Binti wa Kitaa kupinga swala hilo.
Bwana Makundi kuroka Radio France RFI akielezea namna baadhi ya Nchi zenye machafuko zinavyo wanyanyasa mabinti wadogo wenye chini ya umri wa miaka 18 kwa kuwaoa, kufanya nao ngono pia kuwahusisha katika mashambulizi mbalimbali, Pia alieleza kuwa vyombo vya Habari vina jukumu kubwa sana la kuhakikisha jamii inapata taarifa na elimu juu ya kupinga mimba na ndoa za utotoni.
Picha ya pamoja. Picha zote na Fredy Njeje.

No comments:

Post a Comment

Pages