Dande Contact

TEMBELEA BLOG HII KWA MATUKIO YA KILA SIKU-MOBILE +255 713 623 958 / +255 784 623 958 EMAIL dande15us@gmail.com

Halotel


CRDB

CRDB
.

Pages

ASHIKILIWA NA POLISI KWA KUMKASHIFU MSICHANA MWENYE ULEMAVU

Na Talib Ussi, Zanzibar

Kijana  Ame said Khamis (25) mkazi wa Madungu Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba, anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumkashifu msichana mwenye ulemavu wa miguu (21) kwa kumvua nguo kwa dhamira ya kutaka kumbaka.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Pemba Sheikhan Muhammed Sheikhan alieleza kuwa kijana huyo alifanya tendo hilo wakati wa usiku wa saa 2 usiku karibu na Nyumba yao siku ya tarehe 27.

“Tumemkamata kwa sababu tuhuma dhidi yake ni ambalo ni kosa kisheria”.

“Tunashkuru sana kwamba tulipomfikisha hospitali tuliambiwa kwamba hakuwahi kumbaka na chakusikitisha zaidi huyu msichana ni mlemavu, angembaka angemsababishia matatizo zaidi”, alieleza Kamanda huyo.

 Kamanda huyo aliwataka vijana waache tabia ya kukaa kwenye vigenge vinavyojishughulisha na madawa ya kulevya  ambayo ndio yanayopelekea kufanya vitendo ambavyo havikubaliki katika jamii.

Alieleza kuwa matukio mengi ya ubakaji na udhalilishaji hufanywa na watu wale ambao muda mwingi hutumia madawa ya kulevya.

Sambamba na hilo kamanda huyo aliitaka jamii inayoishi na watu wenye ulemavu kuwa waangalifu na watu hao wanaotumia madawa ya kulevya.

Mkurugenzi wa watu wanaishi na Ulemavu Zanzibar  Adil Muhammed alitaka vyombo vya sheria kutenda haki ili kukomesha vitendo hivyo.

“Jamii yetu sisi hua tunapata taabu sana na mkasa huu wa ubakaji kwani watu wengi wanatunayanyasa kwa kila aina ikiwemo ubakaji” alieelza Muhammed.

Vitendo vya ubakaji Visiwani Zanzibar vinaonekana kushika kasi licha ya juhudi kubwa za wanaharakati katika kupambana na vitendo hivyo.

No comments:

Post a Comment