Na Talib Ussi, Zanzibar
Wanaharaka Visiwani Zanzibar wameomba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kupunguza gharama za usajili wa ardhi kwa wanawake ili kuwawezesha kumiliki ardhi ili dhana ya usawa wa kijinsia iweze kufikiwa.
Akizungumza na waandishi wa habari huko Afisini kwake Tungu Mkoa wa Kusini Unguja Mratibu wa Chama cha Waandishi wa Habari wanawake Tanzania upnde wa Zanzibar (TAMWA) Dk. Mzuri Issa Ali alieelza kuwa wanawake wengi wamehamsika katika kujikwamua kiuchumi lakinin kikwazo chao kikubwa ni suala la umiliki wa Ardhi.
Alieleza kuwa gharama za usajili hupindukia tsh: 200,000/- ambazo zinamlolongo mrefu mpaka kupikia kupata usajili kwani mtu anatakiwa apite ngazi nyingi jambo ambalo linawapa ugumu akina mamam unatakiwa uanzi kwa Sheha, Wilaya na hatame Kamisheni ya Ardhi.
“Licha ya hatua hizo lakini mwisho wake unaweza kuona wanawake wananyimwa kwa sababu zisizojuilikana” alieleza Mzur.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa mtandao wa ardhi wa wilaya ya kati Bi Bahati Issa Suleiman alieleza katika kikao hicho katika eneo lake wanawake 107 wamejitokeza kuomba fomu ya umiliki wa ardhi na kati yao ni wanawake sita tu ndiyo waliofanikiwa kukamilisha malipo yote na hivyo kupata hati hiyo.
“Mtandao watu umechukua jitihada za makusudi kuhamamsisha wanawake kumiliki vipande vyao vya ardhi ili kuondosha migogoro ya baadaye lakini tunarudi nyuma kutokana na gharama zinazoambatana taratibu za umiliki wenyewe” alieleza Bi Bahati.
Alisema ni vyema Serikali ikaangalia tena suala hili ili kuzidisha kasi ya maendeleo vijijini kwa jumla na wanawake kwa pekee.
“Ni vizuri Serikali ipitie sera na utaratibu wa ardhi katika mwaka huu mpya ili kuoana na mikataba ya kimataifa na mipango ya nchi ya kuleta usawa wa kijinsia , kupunguza umasikini na kuleta uwiano wa kijamii” alieleza Bi bahati.
Pamoja na jitihada kubwa za kuimarisha ufikiwaji na umiliki wa ardhi kwa wanawake, raslimali ya msingi kwa maendeleo ni kiasi cha asilimia 20 tu ya wanawake ndiyo wanaokisiwa kumiliki ardhi nchin na kwamba kutokana na ukubwa wa gharama hizo, asilimia hiyo itashindwa kuongezeka.
No comments:
Post a Comment