HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 02, 2017

Wanaharakati waitaka SMZ kupunguza gharama ya kumiliki Ardhi

Na Talib Ussi, Zanzibar

Wanaharaka Visiwani Zanzibar  wameomba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kupunguza gharama za usajili wa ardhi kwa wanawake  ili kuwawezesha kumiliki ardhi ili dhana ya  usawa wa kijinsia iweze kufikiwa.

Akizungumza na waandishi wa habari huko Afisini kwake Tungu Mkoa wa Kusini Unguja Mratibu wa Chama cha Waandishi wa Habari  wanawake Tanzania upnde wa Zanzibar  (TAMWA) Dk. Mzuri Issa Ali alieelza kuwa wanawake wengi wamehamsika katika kujikwamua kiuchumi lakinin kikwazo chao kikubwa ni suala la umiliki wa Ardhi.

Alieleza kuwa  gharama za usajili hupindukia tsh: 200,000/- ambazo zinamlolongo mrefu mpaka kupikia kupata usajili kwani mtu anatakiwa apite ngazi nyingi jambo ambalo linawapa ugumu akina mamam unatakiwa uanzi kwa Sheha, Wilaya na hatame  Kamisheni ya Ardhi.

“Licha ya hatua hizo lakini mwisho wake unaweza kuona wanawake wananyimwa kwa sababu zisizojuilikana” alieleza Mzur.

Kwa upande wake  Mwenyekiti wa mtandao wa ardhi wa wilaya ya kati Bi Bahati Issa Suleiman  alieleza katika kikao hicho  katika eneo lake  wanawake 107 wamejitokeza kuomba fomu ya umiliki wa ardhi na kati yao ni wanawake sita tu ndiyo waliofanikiwa kukamilisha malipo yote na hivyo kupata hati hiyo.
  
“Mtandao watu umechukua jitihada za makusudi kuhamamsisha wanawake kumiliki vipande vyao vya ardhi ili kuondosha migogoro ya baadaye lakini tunarudi nyuma kutokana na gharama zinazoambatana taratibu za umiliki wenyewe” alieleza Bi Bahati. 

Alisema ni vyema Serikali ikaangalia tena suala hili ili kuzidisha kasi ya maendeleo vijijini kwa jumla na wanawake kwa pekee.

“Ni vizuri Serikali ipitie sera na utaratibu wa ardhi katika mwaka huu mpya ili kuoana na mikataba ya kimataifa na mipango ya nchi ya kuleta usawa wa kijinsia , kupunguza umasikini na kuleta uwiano wa kijamii” alieleza Bi bahati.
  
Pamoja na jitihada kubwa za kuimarisha ufikiwaji na umiliki wa ardhi kwa wanawake, raslimali ya msingi kwa maendeleo ni kiasi cha asilimia 20 tu ya wanawake ndiyo wanaokisiwa kumiliki ardhi nchin na kwamba kutokana na ukubwa wa gharama hizo, asilimia hiyo itashindwa kuongezeka.

No comments:

Post a Comment

Pages