Dande Contact

TEMBELEA BLOG HII KWA MATUKIO YA KILA SIKU-MOBILE +255 713 623 958 / +255 784 623 958 EMAIL dande15us@gmail.com

Halotel


CRDB

CRDB
.

Pages

WAZIRI MKUU AMJULIA HALI MBUNGE WA KOROGWE VIJIJINI


 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpa pole mbunge wa Korogwe Vijijini, Steven Ngonyani ambaye amelazwa katika hospitali ya Kairuki, Mikocheni jijini Dar es salaam akitibiwa Januari 2, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).


Dar es Salaam, Tanzania


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemtembelea na kumpa pole Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini, Mhe. Steven Ngonyani (Profesa Majimarefu) aliyelazwa katika Hospitali ya Kairuki akipatiwa matibabu.

Akiwa hospitalini hapo leo (Jumatatu, Januari 2, 2017), Waziri Mkuu amesema amefurahi baada ya kumkuta Mbunge huyo anaendelea vizuri na kwamba afya yake inaridhisha.
Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kumtakia afya njema Mhe. Ngonyani. Amesema anaamini hivi karibuni atapona na kuruhusiwa kutoka hospitali.

Kwa upande wake Mbunge huyo ambaye amelazwa katika hospitali ya Kairuki iliyoko Mikocheni jijini  Dar es Salaam, amemshukuru Waziri Mkuu kwa kwenda kumjulia hali.
Pia amesema anaendelea vizuri na anatarajia kwenda nchini India kwa matibabu zaidi mara taratibu zitakapokamilika.


 IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S.  L. P. 3021,
JUMATATU, JANUARI 2, 2017.

No comments:

Post a Comment