HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 21, 2017

Gosbert, ‘Kwa viumbe Vyote’ ndani ya Tamasha la Pasaka

 Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka, Alex Msama, akizungumza na waandisi wa habari jijini Dar es Salaam leo, wakati akitangaza waimbaji waliodhibitisha kushiriki katika tamasha hilo. (Picha na Francis Dande).
 Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka, Alex Msama, akizungumza na waandisi wa habari jijini Dar es Salaam leo, wakati akitangaza waimbaji waliodhibitisha kushiriki katika tamasha hilo.  
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka, Alex Msama, akizungumza na waandisi wa habari jijini Dar es Salaam leo, wakati akitangaza waimbaji waliodhibitisha kushiriki katika tamasha hilo.  
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka, Alex Msama, akizungumza na waandisi wa habari jijini Dar es Salaam leo, wakati akitangaza waimbaji waliodhibitisha kushiriki katika tamasha hilo. 

NA MWANDISHI WETU

WAIMBAJI wa muziki wa injili wamezidi kumiminika kuthibitisha ushiriki wao katika Tamsha la Pasaka litakalozinduliwa April 16 katika Uwanja wa Uhuru, jiji Dar es Salaam kabla ya kuhamia mikoa mingine mitano kuutangaza ufalme wa Mungu na malengo yake mengine ya uwepo wake.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya Tamasha hilo linalofanyika mara ya 17, Alex Msama, alisema ni faraja kwao kuona waimbaji mahiri wakizidi kuthibitisha tukio hilo litakalowaleta na nyota wa ndani na nje ya nchi.

Msama amewataja waimbaji wengine wapya ni Goodluck Gosbert anayetamba na kibao cha Ubarikiwe, John Lissu, Kwaya ya Ulyankulu, moja ya kwaya kongwe na  maarufu iliyowahi kutamba na vyimbo nyingi zenye ujumbe kamili wa neno la Mungu ukiwemo ‘Kwa viumbe Vyote’ unaotikisa hadi sasa.

‘Tunashukuru sana kwani waimbaji wamezidi kuthibitisha kuashiria kuwa maandalizi ndiyo yameshika kasi na wapenzi na mashabiki wa muziki wa injili, wakae mkao wa kupokea Baraka za Mungu kupitia ujumbe wa nyimbo,’ alisema Msama.

Alisema katika uzinduzi wa tamasha hilo utakaofanyika Uwanja wa Uhuru, utakwenda sambamba na uzinduzi wa albamu  ya Kinondoni Revival Kwaya pamoja na kazi albamu mpya ya malkia wa nyimbo za injili nchini na Afrika Mashariki na Kati, Rose Muhando.

“Uzinduzi wa Tamasha la Pasaka April 16 katika Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam, utakuwa wa aina yake kwa sababu kutakuwa na uzinduzi wa albamu mpya mbili; moja ya Kinondoni Revival Kwaya na nyingine Ruthu ya Rose Muhando,” alisema Msama aliyechangia kwa kiasi kikubwa kukuza muziki wa injili kupitia matamasha.

Kuhusu mikoa ambayo Tamasha hilo litapita, Msama alisema baada ya kuzinduliwa jijini Dar es Salaam, mashambulizi yatahamia mjini Dodoma, Mwanza, Shinyanga, Simiyu na kumaliza kazi hiyo mkoani Iringa kwa mwaka huu na kuwataka wadau wa muziki wa injili kuwa tayari kupokea Baraka.

No comments:

Post a Comment

Pages