HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 30, 2017

JUMUIYA YA WATANZANIA WANAOSOMA BEIJING WAADHIMISHA MIAKA 53 YA MUUNGANO

Mwenyekiti wa Jumuiya ya watanzania wanaosoma  Beijing Nchini  Husein Mtoro ( katikati)  aliyemwakilisha Balozi, aliambatana na Viongozi wote Wakuu akiwemo Makamu Mwenyekiti Khamis Ngwali, Katibu Mkuu Ndugu Remidius Emmanuel, Naibu Katibu Mkuu Ndugu Alinanuswe Mwakiluma na Mweka Hazina Ndugu Kulwa Gamba.

Pamoja nao,Viongozi waasisi wa Umoja huo Ndugu Suleiman Serera na Irenius Kagashe nao walishiriki sambamba na Viongozi wastaafu wengine akiwemo Makam Mwenyekiti Mstaafu Ndugu Kassim Jape, Katibu Mkuu Mstaafu Angelina Makoye, Mtunza Hazina Mstaafu Lusekelo Gwassa katika maadhimisho  ya  muungano yaliyofanyika mapema wiki hii kwa kushriki maonesho ya utalii na utamaduni.

Baadhi ya watanzania wanaosoma katika chuo cha Beijing nchini China wakiwa katika maonesho ya utamaduni na utalii kama moja ya maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano  wa Tanzania mapema wiki hii.

Wadau wakipozi kwa picha. 


Maonesho ya utalii na utamaduni  yakiendelea Jijini Beijing.

Picha ya pamoja.

No comments:

Post a Comment

Pages