HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 16, 2018

Benki ya CRDB yanogesha Bonanza Ukonga

NA FRANCIS DANDE

BENKI ya CRDB imetoa vifaa mbalimbali vya michezo kwa ajili ya Bonanza la michezo litakalofanyika kwenye viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji (TCTA),  Ukonga jijini Dar es Salaam.

Vifaa vilivyokabidhiwa ni jezi kwa ajili ya mpira wa miguu, netiboli pamoja na mipira kwa ajili ya timu za chuo hicho.
Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa kukabidhi vifaa hivyo, Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Banana, Albert Michael, alisema kuwa wameamua kutoa vifaa hivyo kutokana na maombi waliyopata kutoka kwa uongozi wa chuo hicho.

“Aidha katika bonanza hilo benki ya CRDB itashiriki kwa njia ya kutoa huduma mbalimbali kwa wanamichezo watakaofika katika bonanza hilo, ikiwemo kufungua akaunti kwa wateja wapya, kuwaunganisha wateja na huduma ya SimBanking, mikopo ya Chap chap kupitia simu ya mkononi ‘Salary Advance', pamoja na mikopo ya kawaida ya wafanyakazi wa muda mrefu kuanzia mwaka mmoja hadi miaka sita,” alisema.

Naye Mkuu wa Chuo hicho, Naibu Kamishna wa Magereza (DCP), Gideon Nkana, aliishukuru benki ya CRDB kwa kuwapatia vifaa hivyo ambavyo vitaongeza hamasa ya mashindano hayo na pia aliitaka benki hiyo kuitumia michezo hiyo kutangza bidhaa zake kwa wadau wa michezo.
Bonanza hilo litashirikisha timu za soka, mpira wa meza, netiboli na wavu. 

Timu zitakazoshiriki kwa upande wa soka ni pamoja na TCTA watakaopambana na Gereza la Keko, KMKGM dhidi ya Chuo Kikuu cha Kampala (KIU), Magereza Dar dhidi ya 511KJ huku Segerea Magereza wakichuana na DIT.

Alizitaja timu zingine ni Taswa FC inayoshirikisha Waandishi wa habari kutoka sehemu mbalimbali watakaowavaa timu ya Ukonga na Kichangani watavaana na Clouds Media.

“Bonanza hili litawakutanisha watu wa tasnia mbalimbali kwa lengo la kufahamiana na kujenga umoja na ushirikiano miongoni mwao, pia kuwaweka watu karibu katika kushirikiana kupitia kazi zao,” alisema DCP Nkana.

Fainali za michuano hiyo zitafanyika kesho kwa kushirikisha timu zote zitakazofanikiwa kuingia hatua hiyo.

Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Banana, Albert Michael, akizungumza katika hafla ya kukabidhi vifaa vya michezo kwa uongozi wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania (TCTA).
Meneja wa Benki ya CRDB, Albert Michael (kushoto), akiwa na Ofisa wa benki hiyo, Esther Metili na Mdhibiti wa Akaunti za Wateja, Elieshi Shoo (kulia), wakikagu vifaa vya michezo kabla ya kuvikabidhi kwa Mkuu wa Chuo cha Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania (TCTA). 
Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Banana, Albert Michael, akimkabidhi vifaa vya michezo, Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania (TCTA), Naibu Kamishna (DCP), Gideon Nkana, kwa ajili ya bonanza litakalofanyika Machi 17 kwenye viwanja vya chuo hicho Ukonga jijini Dar es Salaam.
Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Banana, Albert Michael, akionyesha sehemu ya vifaa vya michezo vilivyotolewa na benki hiyo kwa timu ya TCTA.
Mpira kwa ajili ya timu ya Netiboli.
Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Banana, Albert Michael, akiwa ameshika moja kati ya mipira iliyotolewa na Benki ya CRDB kwa ajili ya timu ya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania (TCTA).
Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania (TCTA), Naibu Kamishna (DCP), Gideon Nkana, akipokea mpira kutoka kwa Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Banana, Albert Michael.
Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania (TCTA), Naibu Kamishna (DCP), Gideon Nkana, akipokea mpira kutoka kwa Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Banana, Albert Michael.
Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania (TCTA), Naibu Kamishna (DCP), Gideon Nkana, akipokea mpira wa timu ya netiboli kutoka kwa Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Banana, Albert Michael.
Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania (TCTA), Naibu Kamishna (DCP), Gideon Nkana, akipokea jezi za timu ya netiboli.
Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania (TCTA), Naibu Kamishna (DCP), Gideon Nkana, akipokea jezi za timu ya netiboli.
Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania (TCTA), Naibu Kamishna (DCP), Gideon Nkana, akipokea maji ya kunywa kwa ajili ya wachezaji.
Jezi za golikipa.
Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania (TCTA), Naibu Kamishna (DCP), Gideon Nkana, akimshukuru Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Banana, Albert Michael.
Picha ya Pamoja.
Ofisa wa Benki, Esther Metili (kushoto), akiagana na
Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania (TCTA), Naibu Kamishna (DCP), Gideon Nkana.

No comments:

Post a Comment

Pages