HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 14, 2018

WAFANYABIASHARA WATAKIWA KUTUMIA BANDARI YA TANGA

Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama katikati akizungumza kushoto ni Afisa Utekelezaji Mkuu wa Bandari hiyo Donald Ngaire na kulia ni Afisa Mipango wa Bandari Moshi Mtambalike
PRO wa Bandari ya Tanga,Moni Jarufu akizungumza katika mkutano huo
Mwandishi wa Habari wa Daily News na Habari Leo mkoani Tanga Cheji Bakari akiuliza swali kwenye mkutano huo
Sehemu ya waandishi wa habari wakichukua taarifa kushoto ni Amina Omari wa Gazeti la Mtanzania mkoani Tanga

MENEJA wa Bandari ya Tanga Privical Salama amewataka wafanyabiashara nchini kuendelea kutumia bandari ya Tanga kwa sababu ina uwezo mkubwa wa kuhudumia shehena kwa haraka kutokana na maboresha makubwa yaliyofanyika.

Salama aliyasema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo alisema bandari hatua yao ya kuhudumia mzigo nangani hakusababishi ikiwa na uwezo mdogo wa kiutendaji .

Alisema hata nchini Singapore bado wanahudumia mzigo nangani na baadae kuleta nchi kavu hivyo wafanyabiashara wanapaswa kutumia bandari hiyo kusafirisha bidhaa zao.

“Bandari ya Tanga kuhudumia mzigo nangani hakusababishi kuwa na uwezo mdogo wa kiutendaji kwani hata nchi ya Singapore bado inatumia kuhudumia mzigo nangani kuleta nchi kavu hivyo niwatake wafanyabiashara kutumia bandari hii kusafirisha mizigo yao“Alisema Meneja Salama.

Alisema Bandari hiyo hivi sasa ina uwezo mkubwa wa kuhudumia wateja ambao watakuwa wakipitisha mizigo kutokana na kuwepo kwa matishari ya kutosha kuhamisha mizigo kati ya gatini na melini nangani inapofika.

“Kwani tunaweza kufanya mzunguko wa nyuzi 360 melini hakuna mashine itakayosimama gatini hivyo kuongeza ufanisi mkubwa wakati wa kuhudumia shehena inayowasili “Alisema.

Hata hivyo alisema bandari ya Tanga ni bora na ina uwezo wa kutoa huduma kwa kasi kutokana na uwepo wa vifaa vya kisasa ambacho vinatumika kufanya kazi hizo kwa wakati Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

No comments:

Post a Comment

Pages