HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 22, 2019

UTT AMIS YADHAMINI MKUTANO WA MAOFISA HABARI SERIKALINI

 Waziri Mkuu akifungua kikao kazi cha Maofisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano Serikalini kilichofanyika Mwanza katika ukumbi wa Benki kuu. Katika ufunguzi huo amewaasa maafisa hao kutoa habari sahihi na kwa wakqti ili wananchi wafahamu wananufaikaje  na taasisi mbalimbali zilicho chini yq Serikali. (Na Mpiga Picha Wetu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akikabidhi cheti cha shukrani Ofisa Masoko na Uhusiano wa Kampuni ya Uwekezaji ya UTT AMIS, Martha Mashiku, kwa kudhamini kikao Kazi cha Maofisa Mawasiliano wa Serikali kilichofanyika Jijini Mwanza kuanzia Machi 18-22.
Ofisa Mwandamizi wa Masoko na Uhusiano wa Kampuni ya Uwekezaji ya UTT AMIS, Rahim Mwanga, akitoa mada kwa Maofisa Mawasiliano Serikalini kuhusu shughuli za kampuni ya uwekezaji na jinsi ambavyo kampuni hiyo imekuwa ikiwawezesha watanzania kushiriki katika uwekezaji kwenye masoko ya fedha na mitaji. Na jinsi ambavyo taasisi hiyo inawawezesha watanzania kujikwamua kiuchumi kuelekea uchumi wa kati mwaka 2025.
Baadhi wq washiriki wa mkutano wa maofisa habari, mawasiliano na uhusiano serikalini wakisikikiliza mada mbali mbali zilizotolewa katika mkutqno huu ambao unafikia tamati Machi 22, 2019.

No comments:

Post a Comment

Pages